Na hii ni nyingine tena! Ona Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya

34Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji.
Nchi jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina hii.
Ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao kutochezwa na vyombo vya habari.
Wakiwa na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku.
35
Screen Shot 2014-08-30 at 2.45.27 PM


Na hii ni nyingine tena! Ona Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya Na hii ni nyingine tena! Ona Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya Reviewed by CapchaMuzic on 08:03:00 Rating: 5
Powered by Blogger.