Huu ndio ujio Mpya wa Diamond baada ya "Kitorondo" Sikiliza Kionjo hapa "Nitampata wapi" Ni sheeda!
Ni mara nyingi Diamond Platnumz huwa anasema kuwa ana nyimbo nyingi sana alizoisha rekodi na bado anaendelea kurekodi kila kukicha, lakini sio nyimbo zote alizonazo zitapata nafasi ya kutoka kama official singles.
Kupitia Instagram yake hit maker wa ‘Number 1’ ameamua kuwaonjesha kidogo mashabiki wake wimbo mmoja ulioko kwenye maktaba yake.
“wakati Mwingine natamanigi hata mngepata dakika moja tu ya kuskia nyimbo nilizo nazo ndani, … hii inaitwa #Nitampata_wapi? sjui kina @babutale wataitoa lini… maana haipo kabisa katika list ya nyimbo zitolewazo… ila, kwakuwa nyie ni watu wangu wa nguvu nimeamua kuwaibia kidoogo, sjui watanimind!#GermanyWeekEnd.” – Diamond
Huu ndio ujio Mpya wa Diamond baada ya "Kitorondo" Sikiliza Kionjo hapa "Nitampata wapi" Ni sheeda!
Reviewed by Unknown
on
02:07:00
Rating: