HIVI NDIVYO ALIVYO UWAWA KWA RISASI MSAIDIZI WA NABII MWINGIRA...MLIMANI CITY,DAR ES SALAAM
INASIKITISHA! Mchungaji
kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, mwishoni mwa wiki
alimpoteza mkalimani wake, Adson Philip Cheyo aliyeuawa kwa kupigwa
risasi katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya ya aliyekuwa msaidizi wa Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, marehemu Adson Philip Cheyo yakiendelea.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Cheyo alikuwa ametoka katika mojawapo ya matawi ya benki mbalimbali zilizopo eneo hilo lenye shughuli nyingi zilizojaa pilikapilika, akiwa na kiasi cha fedha zinazokadiriwa kuwa shilingi milioni nane.
Baada ya kuchukua fedha hizo, inadaiwa kuwa
mkalimani huyo ambaye hutumiwa zaidi na Nabii Mwingira anapokwenda
kuhubiri nje ya nchi, alikwenda sehemu aliyoegesha gari lake na kuingia,
lakini kabla hajafanya chochote, vijana wawili walitokea na kumtaka
awape fedha alizoshika, kitendo ambacho alikitii.
Lakini
pamoja na kuwapa fedha hizo, vijana hao walimpiga risasi mbele ya mke
wake na kuondoka bila kukamatwa, kitu kinachotia shaka kubwa juu ya
usalama wa eneo hilo lenye kutembelewa zaidi na watu wenye fedha jijini
Dar es Salaam.
Katika ibada ya kumuombea marehemu wakati akiagwa tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya, Nabii Mwingira alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwake na waumini wenzake, lakini wanaamini kilichotokea ni mapenzi ya Mungu na wao watamuombea kila mara.
Waumini wengine wa kanisa hilo walionekana kuwa na majonzi, hasa kutokana na kuwa karibu na marehemu huyo, aliyezaliwa Januari 7, 1970.
HIVI NDIVYO ALIVYO UWAWA KWA RISASI MSAIDIZI WA NABII MWINGIRA...MLIMANI CITY,DAR ES SALAAM
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:00:00
Rating: