Hizi ndizo tuzo zinazomilikiwa na Manispaa ya Moshi kwa usafi.
Ingawa
mwaka huu imepata upinzani mkali kutoka kwa Manispaa ya Iringa ambayo
ndiyo imefanikiwa kuwa namba moja kwa usafi lakini manispaa ya Moshi
imesema kuwa wao bado washindi.
Victoria Simakundi ambaye ni Afisa Afya wa Manispaa ya Moshi amesema
kuwa vigezo viliyoweka vya usafi havihusu usafi tu moja kwa moja kuna
masuala ya bajeti pamoja na masuala ya kuweka vitu vipya vya usafi.
Ameongeza
kwa kusema Manispaa ya Iringa walikua chini hivyo kuna vitu ambavyo
wameweza kuvipata kwa sasa na vinaonekana vipya lakini vitu kama hivyo
Manispaa ya Moshi walishavifanya siku za nyuma.
Kuhusu watu wanaochafua Manispaa ya Moshi kuna adhabu amabazo
wameziweka ambazo zinaanzia kiasi cha 10,000 hadi 50,000,Manispaa ya
Moshi imeshika nafasi ya pili mwaka huu baada ya Manispaa ya Iringa.
Tangu mashindano haya yaanzishwe mwaka 1984 Manispaa ya Moshi imekuwa
ikishika nafasi ya kwanza na katika miaka yote,ingawa imeshika nafasi
ya pili mara mbili katika miaka hii 30 ya mashindano haya.
Picha za tuzo zilizopata manispaa ya Moshi mpaka sasa.
Hizi ndizo tuzo zinazomilikiwa na Manispaa ya Moshi kwa usafi.
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:28:00
Rating: