HATIMAYE TORRES AONDOKA CHELSEA, AENDA KUZIBA PENGO LA BALOTELLI AC MILAN
HATIMAYE mshambuliaji Fernando Torres amemaliza miaka yake mitatu na nusu migumu Chelsea kwa kukubali kuhamia AC Milan.
Mchezaji
huyo wa Hispania anakwenda kuziba pengo la Mario Balotelli ambaye Milan
imemuuza kwa Pauni Milioni 16 Mtaliano huyo Liverpool.
Wakala
wa Torres alifanya mazungumzo na Milan Alhamisi asubuhi na mshambuliaji
huyo amekubali kujiunga na vigogo hao wa Italia kwa miaka miwili.
Amechuja:
Licha ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 50 kutoka Liverpool, Torres
amemudu kufunga mabao 45 tu katika mechi 172 alizocheza Chelsea
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anahamia San Siro kwa mkopo wa miaka miwili.
Torres
aliyetua Stamford Bridge kwa dau la Pauni Milioni 50 alikuwa amebakiza
miaka miwili katika mkataba wake wa Pauni 150,000 kwa wiki Stamford
Bridge na inaaminika wawakilishi wake walipatana kiasi hicho hicho cha
mshahara kabla ya mchezaji huyo kukubali uhamisho huo.
Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa radhi kumuacha Torres kabla ya
dirisha la usajili kufungwa Jumatatu ili kupata nafasi ya kusajili
mshambuliaji mwingine na Loic Remy sasa yupo kwenye nafasi nzuri ya
kutua Magharibi mwa London kutoka Queens Park Rangers.
REKODI YA FERNANDO TORRES...
Atletico Madrid (2001-2007) Mechi 244, mabao 91
Liverpool (2007-2011) Mechi 142, mabao 81
Chelsea (2011-2014) Mechi 172, mabao 45
Timu ya taifa Hispania tangu 2003; Mechi 110, mabao 38
HATIMAYE TORRES AONDOKA CHELSEA, AENDA KUZIBA PENGO LA BALOTELLI AC MILAN
Reviewed by CapchaMuzic
on
15:41:00
Rating: