Flora Mbasha Nina Mimba ya Mbasha sio Gwajima....Haya ndio Maswali Magumu aliyojibu Leo

Muimbaji wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha amefunguka mengi kuhusiana na kesi ya mume wake Emmanuel Mbasha pamoja na mchungaji Gwajima ambaye alidaiwa kuwa chanzo cha ugomvi wao.
Frora aliwa na
Kupitia Kikaango ya EATV, ambayo humchukua msanii na kumpatia nafasi ya kuchat na mashabiki wake kupitia ukurasa wao wa Facebook, leo Flora alifanikiwa kujibu maswali mbalimbali kama ifuatavyo.
Jabiri Hayasi:Ni kweli unatoka kimapenzi na Pastor Gwajima maana kuna tetesi kuwa yeye ndiye aliyekushawishi uame kwako uende kwake?.
Flora Mbasha’s Music
Mimi sio mwanamke mpumbavu, nina akili timamu na ninajitambua, zaidi ya yote ninamheshimu Mungu na Kumwogopa Mungu sana.
Frank Meza :Kaa na mumeo hakuna mwanaume utakuja kupata kama yy. Mambo ya nyumbani kwako usipende kuyaanika wazi. Umekaa Naye toka lini? Kumbuka mnamjengeana mazingira gani?

Flora Mbasha’s Music

Ushauri wako ni mzuri sana, lakini kwa jambo usilolijua ni bora kutuombea tu.. swala la hutapata mume kama huyo ajuaye ya sirini ni Mungu pekee, na Mungu anasema, ninayajua mawazo nikuwaziayo asema Bwana, ni mawazo mema sio mabaya, kukupa tumaini
Hassan Matipwili:Kwann ulikimbilia kwa Gwajima badala kwa wazazi wako?
Flora Mbasha’s Music
wazazi wangu walisha fariki dunia, babaangu nilimzika nikiwa mdogo na babu aliyekuwa akinilea nimemzika mwaka jana, kwa hiyo ni mimi na Mungu wangu tu. wala sikukimbilia kwa Gwajima. nasikitika kwa sababu watu wengi mnapenda kuamini maneno ya udaku. ni bora kukaa kimya na kuniombea
Maku Jerry Chambo: Mi sipendezwi na habari za media tofauti kuhusu wewe, labda ufunguke ni kweli au? Vp khxu lile jumba na gari, na kuhusu kumkimbia mumeo?

Flora Mbasha’s Music

Habari hizo sio za kweli na ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili
Mchungaji Peter Severini :Ni Sababu Zipi Zilikufanya Usiende Mahakamani Mumeo Alipopandishwa Kizimbani?
Flora Mbasha’s Music
je ni sababu zipi zilizomfanya mme wangu apandishwe kizimbani..?

Mtasingwa Kitula
:Nilikuwa nakuheshimu na kuthamini kazi yako kumbe we ni wakala wa shetani na umezalilisha walokole wote kwa kuzini nje ya ndoa kisa pesa kweli we mama umelaaniwa na ninakuchukia sana
Flora Mbasha’s Music
Usihukuku usije ukahukumiwa wewe, kuna watu wengi hawataingia mbinguni kwa kuhukumu wasio na hatia.. maneno ya kusikia sikia sio ya kushadadia ni bora uone mwenyewe kwa macho.. lakini hata hivyo ninashukuru kwani kila mmoja anahisia zake sio kosa lako, ila naamini hata wewe ulishakutwa na majanga ya kusingiziwa kama yalivyonikuta mimi.
Flora Mbasha Nina Mimba ya Mbasha sio Gwajima....Haya ndio Maswali Magumu aliyojibu Leo Flora Mbasha Nina Mimba ya Mbasha sio Gwajima....Haya ndio Maswali Magumu aliyojibu Leo Reviewed by CapchaMuzic on 09:21:00 Rating: 5
Powered by Blogger.