Bibi wa mjini Songea ajitengenezea jeneza ili akifa azikwe nalo
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea
Mkoa wa Ruvuma,Bibi Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi
maisha dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali
ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza
alilojiandalia.

Bibi Scholastica akiwa kwenye jeneza alilojiandalia
“Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
“Nimetengeneza kabisa jeneza langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka ili kuepukana na mateso haya. Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa masikitiko.
Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja.
“Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” anasema.
Source:Mwananchi

Reviewed by Unknown
on
09:08:00
Rating: