AY AZUA GUMZO, SOMA HAPA TUKIO ALILOFANYA AMBALO HAKUNA MSANII WA BONGO AMEWAHI FANYA
Kati ya watu wenye bahati unaweza kusema kuna watu wamekuwa nayo toka
wanazaliwa, hii ni mpya kabisa, AY akiwa ndio msanii wa kwanza
kuitangaza Tanzania kimuziki huko ughaibuni, na ndipo wakafuatia na
wasanii wengine kibao ambao hadi hivi sasa wanaendelea kuitangaza
vizuri, ukiachia mbali kuwa yeye ndio anayeongoza kufanya colabo za
muziki na wasanii wengi sana wa nje za nchi.
Hii hapa ni kali zaidi, AY anaweka historia akiwa kama msani wa kwanza
wa Bongo fleva kukanyaga ikulu ya marekani, hii unaweza kusema ni bahati
ya kipekee kwa kuwa, kuna hata baadhi ya watu maarufu na wasanii
duniani ambao kwao bado ni ndoto kutia mguu ikulu hiyo ya marekani.
Akifunguka zaidi kwa yaliomkuta alisema kwanza, kama yeye kwanza
alidhani kuwa ni utani alipopokea barua pepe ya mwaliko huo, cha
kushangaza zaidi alichotakiwa ni kutovaa suti siku hiyo, inayosemekana
kuwa wakati wa siku kama hizo ni marufuku kuvaa suti katika eneo hilo.
AY ni zaidi ya msanii ambaye anawakilisha Tanzania si kwa muziki wake tu
mkali, unaopendwa na watu wa nchi mbali mbali bali zaidi ni balozi wa
UNICEF anayetambulika na mataifa mbali mbali, kujituma kwake kikazi
ndiko kulikomfikisha msanii huyu kufika level hizo na kuzidi kukanyaga
sehemu adimu kama ikulu hiyo ya marekani.
AY AZUA GUMZO, SOMA HAPA TUKIO ALILOFANYA AMBALO HAKUNA MSANII WA BONGO AMEWAHI FANYA
Reviewed by Unknown
on
03:50:00
Rating: