Angelina Jolie na Brad Pitt wafunga ndoa kimyakimya

Mastaa wa filamu, Angelina Jolie na Brad Pitt wamefunga ndoa kimyakimya Jumamosi iliyopita huko Ufaransa. Taarifa ya ndoa yao imetolewa na msemaji wao.
Kwa mujibu wa Daily Mail, waigizaji hao ambao walidumisha penzi lao baada ya kuigiza filamu ya Mr. and Mrs. Smith walionekana katika uwanja wa ndege wa Nice, Ijumaa iliyopita.
Walitangaza rasmi uchumba April, 2013baada ya miaka nane katika uhusiano na walieleza kuwa hatua hiyo ilikuwa hatua ya ahadi ya maisha ya baadae ‘Promise for the Future’.
Angelina Jolie na Brad Pitt wanatarajia kuanza kushuti filamu yao mpya yenye story ya mahaba ‘By The Sea’ na chanzo kimeeleza kuwa katika filamu hiyo wawili hao wataonesha ukaribu sana wa kimapenzi.
Angelina Jolie na Brad Pitt wafunga ndoa kimyakimya Angelina Jolie na Brad Pitt wafunga ndoa kimyakimya Reviewed by CapchaMuzic on 08:53:00 Rating: 5
Powered by Blogger.