Updates!! TUKIO LA VIUNGO VYA BINADAMU KUKAMATWA DAR-WATU NANE WAKAMATWA

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa jana.Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.

 Mmoja ya Kiungo cha Mguu
 Baadhi ya Mifuko ambamo Maiti izo zilikuwa zimewekwa
 Moja ya kichwa cha Binadamu ambacho kimetolewa katika moja ya Mifuko hiyo


 Umati wa watu wakiwa wanashuhudia tukio hilo muda huu


 Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
 Watu zaidi wakiwa wanaongezeka katika eneo la Tukio

Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa ktk mifuko ya plastiki ktk machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dsm

Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura. 

Mpaka tunaondoka eneo la Tukio Miili ilikuwa imechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa Uchunguzi zaidi, Taarifa kamili itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam.
Updates!! TUKIO LA VIUNGO VYA BINADAMU KUKAMATWA DAR-WATU NANE WAKAMATWA Updates!! TUKIO LA VIUNGO VYA BINADAMU KUKAMATWA DAR-WATU NANE WAKAMATWA Reviewed by Unknown on 06:49:00 Rating: 5
Powered by Blogger.