SIYO BURE DIAMOND PLATNUMZ HIYO ITAKUWA LAANA..!! HUWEZI KUMFNYIA HIVYO BABA YAKO...!! SOMA HAPA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhziYxMgB_g7scMZnPAkLvfNyTKKlLi0aVtrdXTSpuMbZCBje998noDysIo85S7dG-MyrZOSlvVH_fmQ37ZEokAfPvpwxK2ZL-xnoqt98hn9MeL0FnL62fEajcgodZApCvvFf_riujQfXU/s1600/927745_703906746345588_1128614094_n.jpg)
Stori: Erick Evarist na Gladness Mallya
Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh.
milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali,
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa
kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba
miguu bila msaada wowote.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi
Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba
miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato
anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa
wapangaji wachache alionao.
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona
katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota
Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo?
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.
“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,”
kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond
alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na
msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu
Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu
sana.”
MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao
unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata
shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya
staa huyo.
“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba
lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa
nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo
hicho.
UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu
walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond
ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia
kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi
mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.
Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri
wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.
“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take
One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo
ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi
ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo
wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.
MATANUZI YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa
malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza
masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na
asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha
halisi ya baba yake.
“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye
vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi
katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau
siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake
pekee,” alisema jirani huyo.
TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond
amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba
yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi
wowote na mzazi wake huyo.
“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki,
tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,”
kilieleza chanzo na kuongeza:
“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake,
sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa
mtazamo wangu kinachofuata ni laana.
“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na
wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa
muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu
watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”
BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya
kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.
“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia
habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.
“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.
DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake
iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya
akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.
MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao
kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili.
Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa
duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu.
Hatutakiwi kumkosoa!
SIYO BURE DIAMOND PLATNUMZ HIYO ITAKUWA LAANA..!! HUWEZI KUMFNYIA HIVYO BABA YAKO...!! SOMA HAPA
Reviewed by Unknown
on
04:37:00
Rating:
![SIYO BURE DIAMOND PLATNUMZ HIYO ITAKUWA LAANA..!! HUWEZI KUMFNYIA HIVYO BABA YAKO...!! SOMA HAPA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhziYxMgB_g7scMZnPAkLvfNyTKKlLi0aVtrdXTSpuMbZCBje998noDysIo85S7dG-MyrZOSlvVH_fmQ37ZEokAfPvpwxK2ZL-xnoqt98hn9MeL0FnL62fEajcgodZApCvvFf_riujQfXU/s72-c/927745_703906746345588_1128614094_n.jpg)