MSANII KUTOKA TANZANIA AKAMATWA CHINA

Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.
HUKU modo
maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota
jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga),
mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki
wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na
polisi nchini humo.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa
kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa
Hong Kong, China.
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa
mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva,
Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye
Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika
kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa
madawa ya kulevya nchini China
MSANII KUTOKA TANZANIA AKAMATWA CHINA
Reviewed by Unknown
on
06:47:00
Rating:
Reviewed by Unknown
on
06:47:00
Rating: