DIAMOND APEWA ZA CHEMBE LAZIMA AKAE
PAMOJA na kazi yake nzuri kabisa ya
kusikia, inayomfanya binadamu afanye mambo yake vizuri katika
kufanikisha maisha yake, bado sikio ni kiungo kidogo tu kilicho ndani ya
kichwa, kiwe cha binadamu au mnyama mwingine.
Licha ya kwamba viungo vyote ndani ya mwili ni muhimu, lakini vipo ambavyo ni muhimu zaidi, kama ilivyo sikio kwa binadamu.
Hata hivyo, umuhimu huo haukipi kiungo hicho ukubwa wa kukizidi kichwa
kwani chenyewe, achilia mbali sikio, pia kinabeba macho, pua, mdomo,
ubongo, fuvu na sura!
Nimeanza hivi kwa sababu staa mmoja mwenye jina kubwa sana katika muziki
wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ staili yake ya maisha
inanitatiza kidogo, japo hainishangazi. Kijana huyu hana mawasiliano
mazuri na baba yake mzazi, Abdul Jumaa.
Mzee huyu anamlalamikia mwanaye kwamba, licha ya kipato chake kikubwa
anachokipata kupitia muziki, bado hamjali kama ambavyo mzazi anastahili.
Juzikati, alipatwa na matatizo ya kuvimba mguu, lakini kijana wake
akawa bize na mambo yake kiasi cha kushindwa kutoa mshiko kidogo ili
baba yake apate matibabu.
Sina uhakika ni nini hasa tatizo kati yao, lakini kwa uzoefu wa maisha
ya Kiswahili, unaweza kukuta kwamba kutengana kwa wazazi kumechangia.
Kwamba baada ya kuachana, mama aliondoka na mtoto. Huenda, mzee
hakuwajibika kwa kijana wake kama alivyotakiwa.
Haya ni matukio ya kawaida katika familia zetu. Tofauti kati ya baba na
mama husababisha kuwapa matatizo watoto. Wakati mwingine akina mama
hupewa mimba na wanaume kuzikataa, ukiangalia na ugumu wa maisha hivi
sasa, baadhi yao huwatupa au hata kuwaua watoto wao.
Inapotokea mtoto akakua, hupewa simulizi, ama na mama au baba juu ya
kilichotokea. Kuna idadi kubwa sana ya watu leo hii ambao wamekua na
mzazi mmoja, wengine wakiishi kwa wajomba au hata babu na bibi zao.
Katika hali halisi, inauma sana kulelewa na mzazi mmoja kwa sababu yapo
baadhi ya mapenzi unayakosa kutoka kwa mzazi asiyekuwepo.
Diamond amekua akiishi na mama yake pekee. Huenda alipewa simulizi
isiyopendeza kuhusu baba yake naye akaamua kuiamini. Ingawa mwenyewe
amekuwa akisema kuwa aliishi katika mazingira magumu sana kabla ya
kufanikiwa, binafsi simuoni kama kijana aliyetaabika kwa sababu pia
amefanikiwa kimaisha akiwa na umri mdogo vilevile.
Kuishi katika mazingira magumu ni jambo moja na uhusiano na mzazi ni
kitu kingine. Kuna vijana wenzake wengi tu mtaani ambao wanaishi katika
mazingira magumu hadi leo, lakini wakiwa na wazazi wao wote wawili.
Maana yangu hapa ni kwamba hakuna uhusiano kati ya magumu aliyopitia na
kutoishi na baba yake.
Kama nilivyosema hapo juu, huenda Diamond
alipewa simulizi mbaya juu ya baba yake. Najaribu kujiuliza tu, kama
mzee Abdul angekuwa na mkwanja wa maana, hivi huyu jamaa asingemfuata?
Jambo moja nimshauri Diamond, wazazi wanabaki kuwa juu bila kujali matatizo yao.
Kuna watu walitupwa na mama zao, wakaokotwa na wasamaria lakini
walipokua na kujitambua, waliwatafuta mama zao bila kujali simulizi
walizopewa na leo wanaishi nao kwa furaha.
Fedha tunazoambiwa kwamba huyu kijana anazo, si lolote si chochote mbele
ya mzazi. Unaweza kuwa bilionea wa kutupwa lakini kama huna uhusiano
mzuri na wazazi wako ut aonekana huna maana mbele ya watu wenye
busara zao.
Kama unafikiri baba yako mzazi atakuja kukuomba msamaha kwa sababu ya
pesa ulizonazo, nadhani utasubiri sana kwa vile nina uhakika hatakuja.
DIAMOND APEWA ZA CHEMBE LAZIMA AKAE
Reviewed by Unknown
on
03:04:00
Rating: