Nchi hii itasonga mbele hata kama watu fulani wakijitokeza kuzuia

 
Tanzania imemaliza uchaguzi tumempata rais, Ameitisha bunge nalimeanza kuwepo kihalali waliokwisha apa ndio wabunge halali. Wengine ni wabunge wateule. Sijui mmoja akikataa kuapa au akaweka sharti katika kiapo ataitwaje?

Lakini kuna mambo yanasemwa semwa na kusomwa somwa.

1) Mija ni hili la kikundi fulani kutengeneza mazingira ambayo yatamzuia rais kuapa.

2) Ni hizi kuwa wanasayansi fulani waliobobea wamefanikiwa kuiba hotuba ya rais atakayoihutubia bunge na wameishaandika kuwa ina ahadi zisizotekelezeka.

Hili la pili nalipima silielewi, Unajua mtu akija na mbinu mpya ya kuchimba dhahabu tutamsifu kwa sababu amegundua jambo la kuwasaidia watanzania. Mtu akija na habari kuwa kuna meno ya tembo yanatoroshwa nchini au dhahabu au kama hayo mengine tutamsifu kuwa mwandishi makini wa uchunguzi na uchunguzi wake una manufaa kwa taifa hili.

Sasa huyu mgunduzi aliyegundua hotuba ya rais ambayo kwa vyovyote vile rais ataisoma hadharani anataka tumshangilie kuwa anafaida gani kwa taifa hili?

kama aliweka jina lake kwenye gazeti itamfaa akijisikia vibaya kuwa hana maana kumbe. Uchunguzi wake hauna faida. Ni sawa anayetabiri kuwa huyu mama mwenye mimba atazaa mtoto.

Hili la kwanza nalo linaweza kumsaidia rais kuwasaidia wananchi waliowachagua watu hao kwenda bungeni kujisahihishadhani nchi inaweza kufanya moja kati ya mawili.

1) Speaker anaweza kuwaita ndani askali ambao watakuwa wameandaliwa ili mradi waingie bungeni na nguo za askari wa bunge. Wawatoe watu hao waliosimama kumzuia rais bila kujali kama watafikishiwa Muhimbili au popote katika kuwatoa nje. Baada ya hapo rais atakayekuwa ameombwa kutoka kidogo kwanza atarudi bungeni na kulihutubia. atakachogundua ni kuwa sura fulani zilizokuwemo hazimo.

2) Njia ya pili ni rais katika kelele hizo kutamka kuwa bunge limezinduliwa halafu akatoka nje huko nje akalihutubia taifa kupitia luninga zote na vituo vya radio, Kuwaelezea watanzania umuhimu wa bunge na wajibu wake katika kuisaidia serikali kuwatumikia wananchi. na kuwa ameshindwa kuongea na wabunge wote kwa sababu watu fulani walimzuia kuongea na wabunge wazuri.

Baada ya hapo awaeleze aliyotaka kulieleza bunge. Awape muda wananchi kuamua la kufanya kama wabunge hao wataendelea kufanya hivyo. Serikali itaendelea kuandaa mipango na kuileta bungeni. Wananchi wataelewa mambo mengi moja ni umuhimu wa kuendelea kukipa wabun ge wengi chama tawala na huo utakuwa mwisho wa vyama vya upinzani.

Tusubiri kuona kitakachotokea kama kitakuwa tofauti na nililosema.

Elisa
Wanabidii google group
Nchi hii itasonga mbele hata kama watu fulani wakijitokeza kuzuia Nchi hii itasonga mbele hata kama watu fulani wakijitokeza kuzuia Reviewed by CapchaMuzic on 07:44:00 Rating: 5
Powered by Blogger.