Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta
Watu wametishwa. Watu wametishika. Makada watakosa za watoto ada. Kujenga kutasimama. Miradi itapigwa radi na kuishia kuwa ahadi. Chama kina utawala wake. Chama kina Mwenyekiti wake. Si huyo Rais wa Tanzania. Kwanini majipu ya chamani nayo yapaniwe kutumbuliwa?
Tumepata taarifa, isiyo na ya kuvutia sifa,kuwa jamaa anataka kupewa nafasi ajinafasi kuyatumbua majipu ya chamani. Lakini, ameombwa asubiri wakati wake ufike. Makada wanakipenda chama kwa 'maslahi yanayoleta uhai'. Yakikaushwa ghafla,hapatatosha. Lakini, Ofisi Ndogo za CCM Lumumba hapakaliki. Hakuna raha ila karaha kusubiri pigo la ghafla.
Makada nchi nzima wanamuunga mkono Rais kutumbua majipu pengine lakini si chamani. Chamani kunafukuta kwa hofu ya 'bifu' kuporwa mnofu. Makada wanatumikia chama na wao wenyewe. Wanatamani wale waminywe na wao wasiguswe ili wasisuse. Hawataki sera ile ifike humu chamani.
Serikalini sawa, chamani si sawa. Double standards!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Lumumba hapakaliki, CCM kwafukuta
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:00:00
Rating: