Wife Kanibambaa na Condom Moja, Sasa Anataka Kujua Mbili Zilikwenda Wapi

Wadau na wakuu wote hapa Jf amani iwe kwenu, nimekaa pembeni kwa muda
mrefu kidogo kutokana na kuwa bize kwenye kipindi hiki cha kampeni
lakini nimekuja hapa kwa dharula tu.
Nimekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya ushindi kwenye kampeni ktk jimbo
flani ambalo lipo ndanindani sana, baada ya kukaa kwa kwa zaidi ya mwezi
nikiwa nje ya mji juzi wife kaja kunitembelea akiwa kaongozana na mke
wa mgombea maana familia zetu marafiki, tena ujio wao ni wa kushtukiza
bila taarifa (cku umepandishwa daraja wanasema alini surprise)
Mwanzo tulipoonana alikuwa ni mtu mwenye bashasha tena aliyejawa
muwashawasha, nikajua hapa leo kazi ni moja kuviringishana mwanzo mwisho
usiku baada ya msosi yeye akatangulia kulala sisi tukabaki na vikao
vyetu vya mikakati, saa 6 hivi naingia chumbani namkuta kakaa kitandani
amefura kwa hasira hadi nikapata hofu (hapo nikaona lile tumaini la
kuviringishana linayeyuka taratibu)
Akaniuliza (hapo akataja jina langu halisi, hicho ndo kipimo cha
kuonesha hasira zake ni kuniita kwa jina) kisha akanionesha "condom
nyingine mbili zimeenda wapi" ilikuwa imebaki moja tu! moyo ukafanya
paaaaah! Ujanja wote mfukoni sura ikanishuka halafu nikahisi inapauka
nikahisi kama vile moyo unasinyaa pumzi zikabana moyo ukapoteza mwenendo
wa mapigo yake, kwa kweli alinishtukiza kwa shambulio baya sana.
Tangu siku hiyo hadi alipondoka cku mbili baadae tulikuwa tunalala na
nguo tu, hakuna maelewano jamani hebu nipeni vi mbinu viwili vi3 vya
kumlainisha huyu mtu ikiwemo uongo wa level za juu maana naona anaelekea
kufika kiwango cha mwisho cha uvumilivu wake, nitamkosa hivi hivi hii
ni serious jamani.
Wife Kanibambaa na Condom Moja, Sasa Anataka Kujua Mbili Zilikwenda Wapi
Reviewed by CapchaMuzic
on
07:19:00
Rating:
