Mke wangu amegundua Baba yangu ndio aliyemuua Baba yake katika ugomvi wa mashamba miaka ya 90......Kwa sasa ameamua kutoweka nyumbani na mtoto mmoja

Mimi ni Mtanzania, mzaliwa wa Kanda ya Ziwa umri wangu ni miaka sasa. Namshukuru Mungu nimebahatika kupata elimu japo kwa taabu sana na sasa nafanya kazi hospitali moja ya umma hapa Dar na huu ni mwaka wangu wa tano kazini maisha yanaenda.Nimeoa na nina watoto 2 mapacha wa kiume.

Nakumbuka nilikua darasa la sita,ulizuka ugomvi mkubwa kati ya mzee wangu na jirani yetu ambae ndie baba wa huyu mke wangu kipenzi. Katika huo ugomvi ambao chanzo chake ni mipaka ya mashamba bahati mbaya sana mzee ambae ni baba wa mke wangu alifariki katika mazingira ya kutatanisha kwani alichinjwa na watu wsiojulikana tena mchana akiwa shambani na mkewe pamoja na huyu mke wangu ambae kwa kipindi hicho alikua mdogo sana. Mzee wangu ndie aliehusishwa na kifo hicho kutokana na ugomvi na marehem na baadae akaja kufariki mahabusu kabla hata hukumu haijatoka.

Kutokana na uhasama huo hawa jirani zetu walihama na kwenda kuishi kijiji jirani maana hali haikua nzuri na huu ugomvi ulianza kua wa kiukoo.Wao walizaliwa wawili yeye na dada yake ambae nilikua nimetangulia darasa moja.Mgogoro huo uliniathiri sana kama mtoto na hasa kifo cha mzee ambae nilimpenda sana, zaidi kilichagiza umasikini wa kupindukia hapo nyumbani.

Hata ivo nilisoma kwa bidii na katika mtihani wa darasa la saba nilifanya vizuri na kuchaguliwa kujiunga shule ya sekondari Ihungo iliyoko manispaa ya Bukoba.Kutokana na umbali pia umaskini sikurudi nyumbani hadi nilipomaliza kidato cha nne.Niliumia sana nilipofika na kuambiwa mama amefariki dunia ni miezi mitatu iliyopita.

Nilikaa kijijini hadi matokeo ya kidato cha nne yalipotoka, nilichaguliwa kujiunga kidato cha 5 shule ya sekondari Ndanda iliyoko wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambapo nilihitimu kidato cha sita mwaka.Nilifanya vizuri na kubahatika kujiunga chuo kikuu nikisomea masuala ya afya miaka miwili baadae yaan 2002.

TULIPOTOKA: Nakumbuka nilikua mwaka wa mwisho wa masomo yangu nilitumiwa shilingi laki nane na rafiki yangu ambae tulikutana kipindi tuko advance alitaka nimnunulie madawa kwenye maduka ya madawa kisha nimtumie huko Dodoma ambako ndiko anafanyia biashara zake.Baada ya kuchukua ile pesa benki niliiweka kwenye begi ambalo ndani yake pia kulikua na laptop yangu nilipanda daladala ambayo ilijaza sana abiria,nilipanga niende nyumbani kisha kesho yake niende madukani kununua mzigo wa jamaa.

Sjui nini kilitokea nilichukua begi langu na kumkabidhi binti ambae alivalia sare za shule anishikie,yeye alikalia siti.Baadae kidogo abiria walipungua nikapata siti na kukaa, kutokana na uchovu nilipitiwa na kausingizi nilikurukupuka niliposkia konda anataja kitua ambapo natakiwa kushuka,niliteremka haraka, ile navuka barabara nakumbuka sina begi. Nilihisi kuchanganikiwa, kibaya zaidi laptop yangu ilikua na documents zangu muhimu ili nihitimu.Nilikaa chini machozi yakawa yananilengalenga sikujua pesa ya jamaa ningeipataje.

Nilirudi nyumani maeneo ya Magomeni ambapo nilikua napanga.Ilipita wiki nzima siendi chuo huku nikimdanganya rafki angu kua nimeshanunua mzigo nitamtumia. Katika kueleza huo mkasa wangu kwa rafiki yangu mmoja aliniuliza unakumbuka huyo binti alivaa sare za rangi gani, nilimtajia japo sikuwa na uhakika sana akanambia huyo atakuwa mwanafunzi wa Jangwani kesho twende. Kesho yake saa kumi na mbili asubuhi tulikua maeneo ya shule tukimwangalia kila mwanafunzi wa kike anaeingia na kutoka ila hatukuambulia kitu, kibaya zaidi nilkua sina uhakika na sura ya binti mwenyewe.

Tulikata tamaa maana tulirudia zoezi kwa siku mbili bila mafanikio. Wiki ya pili tangu begi lipotee nilipigiwa simu na yule rafiki yangu akanambia ana mshikaji waka ni mwalimu pale Jangwani ameongea nae anasema kesho twende atatangaza parade kama tuna uhakika ni mwanafunzi wao ndie aliondoka na begi.Tulifika, kweli wanafunzi wengi walikuepo walitangaziwa kisha sisi tukaondoka.

Siku ya tatu nikiwa chuo nilipigiwa simu na yule mwalimu akanambia niende shuleni.Nilifika hapo shuleni nikakutanishwa na mwalimu wa zamu na wa nidham ambao walinambaia kuna mwanafunzi anao huo mzigo.Aliitwa, akanambia begi analo ila amemwachia mjomba wake amba anishi nae, kwakweli sikuamini macho yamgu nilibaki namtazama yule binti ambae kwa wakati huo alikua kidato cha nne nilijikuta namkubatia bila kujali walimu wake. Nilikabidhiwa kwa mwalimu wa zamu ambae tuliambatana na huyu binti hadi kwao, alikuwa anaishi Gongo la Mboto.

Mjomba wake alinikabidhi begi na pesa yote ikiwemo,alikua ni mzee sana ila mwenye busara nyingi, nyumba iliyochoka isiyo hata na umeme. Nilishangaa sana. Kuanzia siku hiyo nilijikuta nimetokea kumpenda sana yule binti lakini kitu nilichogundua haraka sana alikua ni mtoto wa jirani yetu ambae alikua na mgogoro na marehemu baba kabla hajafariki.

Hili nililigundua kutokana na yeye kufanana na dada yake ambae tulisoma wote primary ingawa sasa nilikuja kujua kua nae alishafariki, pia mama yake alishafariki.Kiukweli alikua binti mmoja mzuri sana yaan mrembo hasw japo maisha magum yalificha yote. Nilibahatika kumaliza chuo mwaka 2008 na yeye akamaliza kidato cha nne. Bahati mbaya hakufaulu vizuri. Nilishampenda sana mwaka 2010 tulifunga ndoa takatifu.

MADA KUU:
Tumeishi kwa amani, furaha na upendo wa hali ya juu huku kipato nacho kikizidi, ila kwa vile nilimpenda sana na kwa kuhofia asije kujua historia halisi ya maisha nilimwambia kwetu ni hapahapa Dar na kumtambulisha mzee mwenye nyumba Magomeni nilipokua naishi kipindi nasoma kama baba yangu na aliamini hivo, nae huyo mzee amefariki mwaka juzi. Nimekua nikiishi ndugu zangu halisi kiujanjaujanja na nilipotaka kwenda kwetu ilibidi niende kwa kujificha sikuwahi kuambatana na mke wangu.

Sasa mwezi huu mwanzoni alifariki yule mjomba wake ambae alikuwa akiishi naye. Kwa kweli nimekuwa sijihusishi na mikusanyiko yoyote ambayo inanikutanisha mimi na familia yake na mara nyingi natoa sababu au nasafiri ghafla; Kwenye huu msiba ndipo yalipoibuka yote na yeye akafahamu kila kitu. Alilia sana, nilibembeleza lakini wapi.

Ni wiki sasa tangu atoweke nyumbani na mwanangu mmoja. Nimemtafuta kila mahari simpati. Maisha yamevurugika mtoto anauliza alipo mama mama mi namwangalia tu.

Hata siku moja hatukuwahi kukwaruzana nampa kila anachotaka, ni mwanamke mkimya sana na mwenye upendo wa kweli sijui kwa hili itakuaje.
Mke wangu amegundua Baba yangu ndio aliyemuua Baba yake katika ugomvi wa mashamba miaka ya 90......Kwa sasa ameamua kutoweka nyumbani na mtoto mmoja Mke wangu amegundua Baba yangu ndio aliyemuua Baba yake katika ugomvi wa mashamba miaka ya 90......Kwa sasa ameamua kutoweka nyumbani na mtoto mmoja Reviewed by CapchaMuzic on 10:03:00 Rating: 5
Powered by Blogger.