Nilipewa Hirizi Nikaimeza, Nilitaka Nikitongoza Wanawake Nisikataliwe. Hali imekuwa Mbaya Sasa, Dada Yangu wa Damu Ananitaka Sasa
Natumaini mko poa,nilipokuwa kijana na balehe nilikuwa napenda sana
wasichana, yaani nilikuwa natamani sana wanawake wazuri wote wawe wangu,
siku mmoja niliposafiri kwenda kijijini kwetu, nikakutana na vijana wa
kule kijijini tulikuwa tunapiga story kuhusu mambo ya wasichana, ndipo
tukafikia hizo story za kutumia madawa kuwavutia wanawake ndipo kijana
mmoja akaniambia babu yake ana dawa nzuri sana ya hizo mambo.
Kwa
vile kipindi kile nilikuwa napenda sana wasichana nilimwambia anipeleke
kwa babu yake nikachukue hiyo dawa, nilipofika kule nikamwambia yule
babu shida yangu ya kupata dawa ya mvuto kwa wasichana, yule babu
akaniambia ana dawa mbili ya kuoga na ya hirizi nichague ipi, nikachagua
ya hirizi, akaniambia natakiwa nimeze hiyo hirizi ndogo na akanipa na
dawa ya maji ninywe ikiwa imechanganywa na damu sijui ni ya mnyama gani.
Baada
ya kumeza hirizi na kunywa ile dawa ya maji, yule babu akaniambia
kuanzia siku hiyo hakuna mwanamke atakaye nikataa nikimtongoza. Sasa
imepita miaka kumi na moja, sijawahi kukataliwa na mwanamke yoyote
niliyemtongoza na nimeshakula pesa za wanawake wengi.
Sijawahi
kumuomba hela mwanamke akaninyima labda asiwe nayo. Sasa hivi juzi
kati, dada yangu nae ameanza kunitongoza anadai anavutiwa na mimi
kimapenzi, anasema amevumilia sana ameshindwa imebidi aniambie, najaribu
kumuepuka lakini wapi.
Jamani hii dawa inanitesa sana, najuta kuitumia. Imenifikisha pabaya.
Naombeni ushauri wenu.
Nilipewa Hirizi Nikaimeza, Nilitaka Nikitongoza Wanawake Nisikataliwe. Hali imekuwa Mbaya Sasa, Dada Yangu wa Damu Ananitaka Sasa
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:51:00
Rating: