MAITI YAKOHOA, YAFUMBUA MACHO.......MSIBA WAVUNJIKA
MAITI (1)Tunu Shabani anayedaiwa kuzinduka baada ya kufariki dunia, akiweweseka.
Maajabu
ya Bagamoyo! Katika hali ya kushtua, familia yenye makazi yake,
Magomeni, Bagamoyo mkoani Pwani, imejikuta kwenye mauzauza baada ya
ndugu yao kufariki dunia huku akidaiwa kukohoa, kufumbua macho na
kuonesha dalili za kuwa hai, pamoja na kwamba daktari alithibitisha
kifo.
WAOMBOLEZAJI WATIMUA
Katika
tukio hilo lililosababisha waombolezaji kutimua mbio lililojiri Juni 28,
mwaka huu, binti wa familia hiyo, Tunu Shabani (36), alifariki dunia
katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kutokana na kuumwa kichwa ghafla.
MUME ASIMULIA
Akizungumza
na Amani lililofunga safari kutoka Dar hadi Bagamoyo, mume wa Tunu,
Iddi Ramadhani alisema mkewe alianza kupata maumivu ya sikio baadaye
kichwani ambapo alimhamishia kwa wazazi wake maeneo hayohayo ya Magomeni
kwa kuwa ni karibu na hospitali.
Iddi alisimulia kuwa
Juni 27, mkewe huyo alipelekwa kwenye hospitali hiyo, akatundikiwa dripu
lakini hali ilizidi kuwa mbaya kiasi cha kuwekewa mashine ya kupumulia
kabla ya kuaga dunia alfajiri ya Juni 28.
“Baada
ya daktari kuthibitisha kifo cha mke wangu, ndugu tulikutana, tukaandaa
mazishi kwa kuchimba kaburi na shughuli ya kuandaa maiti kwa ajili ya
mazishi tuliyopanga yafanyike saa 6:00 siku ya pili yake yaani Juni 29.
“Wakati wa kuosha maiti mara tukasikia sauti kasha ikafumbua macho, miguu yake ikajinyoosha na mwili ukawa na joto.
“Ilibidi tusitishe kumzika kwanza na kujaribu kumtafuta daktari,” alisema Idd.
Aliongeza
kuwa, hali ya marehemu iliendelea kuwatatiza kwa kuwa wataalam
walishindwa kufanya chochote hadi Juni 29, walishangazwa zaidi kuona
maiti ikiwa inatoka jasho jingi huku joto likiendelea kuwa vilevile.
MAITI (6)Mashuhuda wakizungumza naye.
SHEHE ANENA
Akizungumza
na waandishi wetu, shehe aliyekuwa akisimamia kuandaa maiti, Mtawa Adam
(pichani) alisema kuwa kwa mujibu wa taratibu za mazishi za Dini ya
Kiislam, marehemu ambaye ni mwanamke huoshwa na wanawake wenzake, kanuni
ambayo mwili wa Tunu nao uliipitia.
Shehe Adam alisema
kuwa, kama kawaida alimpima marehemu na kumshonea sanda huku akisubiria
wanawake hao wamalize kumuosha na kumuandaa ili yeye aingie kwa ajili
ya kumnyosha viungo, lakini kabla hawajamaliza, alishtushwa kuwaona
wakitoka mbio na kudai maiti imefumbua macho na kunyoosha mguu.
MAITI
(5)“Niliingia ndani na kumuona marehemu ambapo wakati huo alikuwa
amefumba macho, nilipomgusa alionekana wa moto kama alikuwa hai,
nikamtazama nyayo zake zilionekana ni nyeupe tofauti na za marehemu
ambazo huwa za njano.
“Nilimrekebisha mguu wake
aliounyoosha, lakini nikashangaa ukirudi tena kama ulivyokuwa awali na
hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga mara moja baada ya dakika
hata mbili,” alisema shehe huyo na kuongeza kuwa aliwashauri wanafamilia
wamuondoe Tunu kwenye kitanda cha maiti na kughairi maziko huku daktari
mwingine akiitwa kumpima lakini naye alisema alifariki dunia.
MAITI (2)Umati ukiwa umefurika.
UMATI WAJAA
Waandishi wetu, walishuhudia umati wa waombolezaji wakiwa wamezunguka eneo hilo ili kushuhudia kilichoendelea.
MAMA APANDISHA MASHETANI
Katika hali isiyo ya kawaida, mama mmoja alipandisha mashetani na kudai Tunu hajafa.
WAGANGA WANNE
Kwa
mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake,
waliwaita waganga wa nne wa kienyeji ambapo mmoja alifika na kudai Tunu
alichukuliwa msukule lakini alishindwa kumfanya awe hai.
Aidha, waganga waliobakia licha ya kufanya ndumba zao, Tunu hakuweza kuamka kama walivyodai awali.
Baba
mzazi wa marehemu, Adam Hassan akizungumza na waandishi wetu alisema
Tunu hakuonesha dalili za kuwa hai hivyo taratibu za mazishi zilifanyika
kesho yake (Juni 30) na kuzikwa katika Makaburi ya Kiwangwa, Bagamoyo.
MAITI YAKOHOA, YAFUMBUA MACHO.......MSIBA WAVUNJIKA
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:34:00
Rating: