Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada......Maana Halisi na Matumizi Yake
Nini Madhumini na matumizi ya vitu vifuatavyo wavaapo wakina dada na akina mama katika jamii yetu,
1: Kipini cha puani a.k.a (Kishaufu) iwe kushoto au kulia
2: Kikuku iwe mguu wa kushoto au kulia au yote kwa pammoja
3: Na mwisho ni Shanga za kiunoni.
Je waona je vyapoteza maana halisi kwa wanao vaaa hole hole hole au?
Maoni yako tafadhali changia
============================== =============
MAJIBU YALIYOPATIKANA
============================== =============
Nimeona nilete mada hii ili kuwekana sawa katika ishu ambayo inaongelewa pasipo kuwa na ufahamu wa kina. Katika mapambo yanayotumika sana ulimwenguni na tena na watu wa marika tofauti ni pamoja na vikuku na vishaufu.
=> Kuhusu vikuku miguuni
Kwa makabila ya kiafrika vikuku huvaliwa kuanzia na watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo na hata vikongwe.
Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi, au hata madini kama dhahabu, fedha na hata shaba. Vyaweza kuvaliwa mguu mmoja au hata miguu yote.
=> Kuhusu uvaaji wa Vishaufu/kipini puaniMiongoni mwa mapambo yanayotumika zaidi na wanawake huku umaarufu wake ukiongezeka siku hadi siku ni urembo aina ya vikuku, ambavyo huvaliwa miguuni.
Awali urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.
Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.
Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.
Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao ni wadau wa urembo wanafafanua kuwa pambo hilo halina maana yoyote livaliwapo kwenye miguu ya mwanamke zaidi ya urembo kama ilivyo kwa hereni na mikufu.
“Watu wanashindwa kuelewa kuwa kikuku ni urembo wa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine, mfano bangili, hereni, cheni ya shingoni, pete ,vidani na mapambo mengine ambayo hupenda kujiweka mwilini, unajua mwanamke kujipamba,”anasema Nice Siema
Anafafanua kuwa uvaaji wa urembo huo hauwezi kutafsiri tabia ya mtu kwa kuwa ni pambo kama yalivyo mapambo mengine yanayotumiwa na wanawake.
“Unajua siku zote wanawake wanapenda kupendeza ndiyo maana huwa na furaha kama sehemu kubwa ya miili yao wataiweka urembo tunaona hata vidole vya miguu vinavalishwa pete hiyo yote ni urembo tu hakuna maana yoyote mbaya,”anasema Siema
Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.
Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.
Tukirudi kwa vishaufu, urembo huu ambao huvaliwa puani aghalabu hupatikana kwa makabila ya pwani lakini kwa miaka ya karibuni umeenea hata kwa makabila mengine hasa kwa wasichana.
=> Kuhusu uvaaji wa shanga kiunoni
Hitimisho
Kwanini basi naleta hii ishu tuijadili ni kwamba, hapa JF nimesoma baadhi ya wachangiaji wakihusisha hasa vikuku na mienendo isiyofaa na kuleta dhana kuwa wenye kutumia mapambo hayo basi wana ajenda nyingine.
Binafsi napenda kusema kuwa urembo wowote waweza kutafsiriwa vyovyote - kwa ubaya au uzuri ila mwisho wa siku mtumiaji/mvaaji tu ndiyo mwenye kujua maana.
Wenzangu sijui mnasemaje?
Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada......Maana Halisi na Matumizi Yake
Reviewed by CapchaMuzic
on
07:49:00
Rating: