BAADA YA KUDAI ANAOLEWA HIVI KARIBUNI, HIKI NDICHO KILICHOTOKEA NDO YA LULU
BAADA
ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014, mwigizaji Elizabeth Michael
‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu
mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye
anayewezesha kila kitu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi
karibuni, Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo
suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala
hilo na anaamini litakuja kutimia.
“Ndoa ni mipango ya
Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna
mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,”
alisema Lulu.
Akizidi kupiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema
kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna
mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani
baada ya miaka miwili ijayo.
‘Lulu’ akipozi.
“Sina mpango
hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita
ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.
Alipotakiwa
kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini
akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.
“Kwanza
nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya
kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee.
Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.
Kuhusu
mikakati yake ya sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea
na masomo huku akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia
kuzifanya.
“Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi,” alisema Lulu.
BAADA YA KUDAI ANAOLEWA HIVI KARIBUNI, HIKI NDICHO KILICHOTOKEA NDO YA LULU
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:36:00
Rating: