Wema : Diamond Anakinyongo na Mimi!

Akiongea redioni kwenye kipindi cha Ubaoni cha EFM hapo jana , Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu alisema kuwa hana kinyongo na aliekuwa mpenzi wake, Diamond ambae ni staa wa Bongo Fleva, ila Diamond ndiye bado ameendelea kuwa na kinyongo naye.
Wema alisema kuna siku alimtumia ujumbe wa simu Diamond kumpa pole kwa kumuuguza mama yake lakini alimchunia.
“Tumeshaachana kwanini tuwekeane grudges,?”alihoji Wema kwenye kipindi hicho. “Tulikuwa pamoja lakini tumeachana kwanini tuwekeane bifu, kinyongo?

Kwahiyo kama ulikuwa na mtu halafu mkaachana hamtakiwi kuwekeana kinyongo,” alisisitiza.
“Mimi siwezi kuwa na kinyongo na Diamond hata siku moja lakini imekuwa iko tofauti kwa sababu mwenzangu hayuko hivyo anataka ile no! No! sijui ni kwa nini lakini labda kila mmoja ana jinsi anavyofikiri.”
“Sijawai kumpigia simu ila nilishawakumtext, nilisikia kwamba mama yake anaumwa baada ya kusikia mama yake anaumwa nilim-text kama pole kwa sababu sina kinyongo naYe nikampa pole lakini kama nilivyoowambia mwenzangu yupo tofauti, nilifanya kibinadamu yule mama mimi hajanikosea.”
Wema : Diamond Anakinyongo na Mimi!
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:51:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
08:51:00
Rating: