Utata wa video ya Mchungaji iliyozagaa mitandaoni akiwa UCHI Afrika Kusini
Mchungaji maarufu Afrika Kusini Sthembiso Zondo ambae huwa anatoa
mahubiri yake kwa njia ya Redio nchini humo, ratiba ya kurushwa kwa
mahubiri yake imesimamishwa kurushwa hewani baada ya kuvuja video
inayomuonyesha akizungumza kwenye simu huku akiwa hajavaa nguo yoyote.

Shirika la utangazaji la Afrika Kusini (SABC) limetoa amri ya
kusimamishwa kwa Kipindi cha mchungaji huyo hadi itakapotangazwa tena,
maamuzi yaliyotolewa baada ya video inayomuonyesha Mchungaji Zondo akiwa
hajavaa nguo iliyowekwa kwenye mitandao. Video hiyo inaonyesha kuwa
ilirekodiwa na mwanamke aliyekuwa amevaa skirt ya pink lakini hakuweza
kutambulika.
Taarifa zinasema kuwa Zondo aliomba radhi kutokana na kuvuja kwa video
hiyo, japo kulikuwa na mvutano pia wengine wakilaumu aliyevujisha video
hiyo huku wengine wakimfata mchungaji huyo ajieleze kuhusu video hiyo.
Video iko hapo chini
Utata wa video ya Mchungaji iliyozagaa mitandaoni akiwa UCHI Afrika Kusini
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:30:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:30:00
Rating: