Sitti Mtemvu sasa kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014 na kuna uwezekano mkubwa akaishia polisi. Soma hapa
WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania
2014, Sitti Abbas Mtemvu, taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea
na taji hilo.
FikraPevu imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua
Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa
kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba
taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu, ambaye ni baba yake.
UNAWEZA SOMA R.KELLY APOST PICHA HII YA ALI KIBA NA KUANDIKA MANENO HAYA
Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
FikraPevu imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18.
Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa
Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za
uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.
Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, ameiambia FikraPevu leo
Alhamisi Oktoba 31, 2014 kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina
kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo
vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa.
Unaweza soma :Mbinu Mpya za Wanawake wa Siku Hizi Wanao Saka Ndoa Kwa Nguvu
Unaweza soma :Mbinu Mpya za Wanawake wa Siku Hizi Wanao Saka Ndoa Kwa Nguvu
Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka
alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza
uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa
chini ya kiapo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa…
Sitti Mtemvu sasa kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014 na kuna uwezekano mkubwa akaishia polisi. Soma hapa
Reviewed by CapchaMuzic
on
07:36:00
Rating: