MNAOPENDA NGONO KINYUME NA MAUMBILE SOMENI HII
NI
matumaini yangu wapenzi wa safu yetu maridhawa ya Love Story mko
vizuri. Tunakutana tena katika maeneo yetu ya kujidai na kupeana mawili
matatu yahusuyo mapenzi.Raha
ya mapenzi ni pale yanapofanyika kwa nafasi na usalama. Kila mmoja
akaendelea kufurahia uhusiano kwa maana ameridhika katika njia ambayo ni
salama kwa pande zote mbili.Ndugu zangu, penzi linanoga pale
linapomhusisha mwanaume na mwanamke katika njia ambazo hazina madhara na
si vinginevyo.
Ukitazama kichwa cha habari hapo juu, suala la watu kuingiliana
kinyume na maumbile ni tatizo ambalo linaendelea kushamiri kwa kasi kama
moto wa kifuu siku hadi siku katika kizazi cha sasa.
Linaonekana kuzoeleka na watu kutaka kulifanya la kawaida au kusema ndiyo fasheni ya kisasa. Kweli jamani!
Linaonekana kuzoeleka na watu kutaka kulifanya la kawaida au kusema ndiyo fasheni ya kisasa. Kweli jamani!
Utasikia binti akikwambia kwamba bila kufanywa tendo hilo hajisikii
raha. Anasema hivyo kwa sababu ya mazingira ambayo ameyapitia maishani,
simlaumu kwa sababu tatizo hilo limehamia hadi kwa wanaume, kutokana na
mazingira waliyoyapitia nao sasa wapo ambao hawasikii raha bila kufanya
tendo hilo.
Utasikia mwanaume anakwambia bila kufanya kinyume na maumbile hasikii
raha. Tatizo linakuwa hapo, anayependa kufanya mchezo huo akikutana na
ambaye hapendi kufanya huwa unaibuka ugomvi na madhara yake inakuwa ni
ugomvi kila kukicha.
Wanawake wengi wamekuwa wakinitumia ujumbe mfupi wakiniambia jinsi
wanavyopata usumbufu kutoka kwa wanaume ambao wanapenda hako
kamchezo.Wengi wamesema huwa wanakataa lakini wanaume huwa wabishi na
wakati mwingine hufanya tendo hilo kwa kulazimisha au kujifanya
wamekosea.
Historia inaonesha kizazi cha mababu zetu, mchezo huu haukuwa
ukifanyika lakini vitendo hivi vimeshamiri kwa kizazi cha sasa kutokana
na ujio wa DVD za ngono kutoka nchi za magharibi.
Watu wameona, wakakopi na kupesti katika uhalisia na kuona yanafaa. Wakaanza kuyatumia tena wakanogewa kiasi cha kusema: “Mimi bila kinyume na maumbile, sijainjoi mahaba.”Taasisi moja ya Kimarekani imetoa taarifa kwamba licha ya magonjwa mengi ambayo yanaweza kusababishwa na tatizo la kuingiliana kinyume na maumbile lakini pia upo uwezekano wa mtu kuweza kuambukizwa kansa. Imeelezwa kuwa, virusi aina ya human papilloma ambavyo husababisha kansa huweza kuhama kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kupitia tendo hilo la kujamiana kinyume na maumbile.
Mbali na hilo, inaelezwa kwamba ni rahisi sana mtu kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi kutokana na msuguano unaosababishwa na ‘nature’ ya mazingira ya eneo husika ambalo halina majimaji ya asili yanayoweza kulainisha kuepusha msuguano ambao unaweza kusababisha magonjwa kusafiri kwa urahisi kupitia damu.

Nini kifanyike?
Licha ya kuwa wapo wataalamu wanaoshauri njia mbalimbali za kufanya ili kuhalalisha aina hii ya ngono iwe salama lakini nikushauri tu msomaji kuacha kabisa mchezo huu maana faida zake ni chache kuliko hasara.

Inatajwa kuwa huweza kuwasababishia wanawake matatizo wakati wa
kujifungua kwa kutenda tendo ambalo linapingana na lile ambalo Mungu
mwenyewe amelipitisha katika njia ya kuzaliana kupitia sehemu ya
kawaida.
Hii ni tabia ambayo iliingia, tuna uwezo kabisa wa kuipinga kwa nguvu
zote kwani raha ya mapenzi ipo katika mfumo mzuri ambao kila mmoja
anaufahamu. Kwa yule ambaye ameshaathirika na mchezo huu, inampasa
kubadilika na kurudi katika njia salama ambayo haina madhara mengi.
MNAOPENDA NGONO KINYUME NA MAUMBILE SOMENI HII
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:56:00
Rating: