Masaa 48 yajayo tunaitazamia Tanzania mpya na viongozi wapya, Thank you Prof. Kikwete

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2010/11/Kikwete.jpgNi kama hayawi hayawi lakini yamekuwa jamani tumesikia mengi sana ila masaa ambayo sii mengi histori inaenda kuandikwa watu wamesha nowa hoja zao mithili ya majambia au viwembe vikali bunge linaenda kuungana maana hoja ya chama cha mapinduzi ni kuwa habebwi mtu hapa tamko limeshatoka na mkuu amekwisha bariki maana ikulu ni taasisi nzito yenye dhamana ya wa Tanzania wote.
Mama Anna makunda hana uwezo na kamwe hatojaribu kuchokoza wabunge kwa kuzuwia mjadala Mama amekujakuhitimisha kazi maana ameshasoma alama za nyakati, mapanga ya hoja yakiwakosa vigogo wa iptl basi hawato muachia hoja yaku mng'oa itaenda kuwekwa mezani na na huo ndi utakuwa mwisho wa u spika wake. Kwa wale wanao fuatilia bunge mmesikia akisema atafanya haraka hoja iletwe mezani watu wakaisome nakufanya maamuzi.
Jambo linalosumbua akili za walio wengi ni vile wahusika wote wamedindisha mpaka sasa jambo linaloleta mashaka makubwa sana.
WAZIRI MKUU
Waziri mkuu akiwa ndio mkuu wa shughuli zote za serikali hataki kuamini wabunge walio mpenda na kumsifia na hata kumbeza waziri mkuu alie wahi kujiuzulu Mh. Lowassa wamemgeuka na kumpa vipande vizito anaamini muujiza utatokea apone ila alama za nyakati zinaonyesha kuwa chini ya uongozi wa Prof J.K hakuna aliyefanya ujinga akapona huyu bwana mkubwa kama mtaikumbuka kauli yake ya mwanzoni kabisa akilihutubia bunge kwa mara ya kwanza aliwahi kusema taasisi yake yani ikulu haina ubia na mtu na ndio maana Lowassa aliwajibika
Sasa hali imekuwa ni nzito kwa Bwana Pinda uwaziri mkuu mtamu na amekuwa mstari wa mbele kuwaadabisha wenzake wakati yeye akipona wanachama wengi wamemuona kuwa ni ndumila kuwili na ndio maana kukawa na mtifuano mkali ktk vikao vya ndani.
Hii subiri subiri ni ilikuwa maandalizi ya kuwaondoa na taratibu zote zimeshamalizika na kazi ni moja tu kuwang'oa kwa nguvu masaa 48 yajayo ukweli utakuwa wazi.
Masaa 48 yajayo tunaitazamia Tanzania mpya na viongozi wapya, Thank you Prof. Kikwete Masaa 48 yajayo tunaitazamia Tanzania mpya na viongozi wapya, Thank you Prof. Kikwete Reviewed by CapchaMuzic on 09:12:00 Rating: 5
Powered by Blogger.