Mama Yangu Amenionyesha Baba Yangu Halisi Baada ya Miaka 38, Nimemkataa Laivu
Mimi
nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia,
nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa
hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba
nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu
nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya
watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki
kuharibiwa maisha yangu.
Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.
Je waungwana nilichofanya ni makosa?
Mama Yangu Amenionyesha Baba Yangu Halisi Baada ya Miaka 38, Nimemkataa Laivu
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:10:00
Rating: