Kwa tabia hizi nani akuoe?
Wewe ni ni msomi kweli sikatai,wewe ni mzuri tena sana sikatai.Una kila kitu ambacho mwanaume yoyote angependa kuwa nawe japo kwa mahusiano ya boyfriend and girlfriend lakini hauna sifa za kuwa mke wa mtu.
Una ndoto kubwa ya kuolewa na kuwa mke wa mtu na ndio maana kila siku hauishi kunikumbushia juu ya ile ya ahadi yangu ya ndoa kwako kabla ya 2015.Mwanzoni nilitaka kutimiza ahadi yangu mapema mwaka huu kwa kuanza na kutoa mahali lakini mtu mmoja akanifinya sikio akaniambia kaka chukua muda zaidi kumsoma,nikamwambia nimeshamsoma kabisa hana tatizo,akaniuliza umetumia njia gani kumsoma nikamtajia ndugu yangu bado haitoshi fanya moja mbili na utaona tabia zake halisi.Kweli nikaufanyia kazi ushauri wa ndugu yangu yule na baada ya muda kweli nikaanzakuiona tabia zake halisi za mrembo huyu.
Mwanamke hata uwe na elimu vipi hutakiwi kuonyesha KIBURI kwa mwenzi wako hasa ikiwa ndio kwanza unatafuta nafasi ya kuolewa.Sasa mrembo huyu wa Mr.Yes kwake yeye ni kitu cha kawaida sana kwake.Mwanzoni sikujua tabia hii ila baada ya kutumia ushauri wa ndugu yangu ndio nikajua hii tabia yake.Hapo nani akuo?mimi Mr.Yes?akuu najiweka pembeni bora nionekane msaliti.
DHARAU ndio haiba yako,ya nini kufanya/kumfanyia dharau mpenzio/hata mtu yoyote yule eti tu kwakuwa u-mzuri na una elimu?hee jamani si unataka mimi Mr Yes nikuoe nikuweke ndani na tuwe bibi na bwana?sasa ikiwa unayafanya haya ingali bado tupo kwenye mahusiano ya kawaida tu tukiingia kwenye ndoa si itakuwa balaa.Mr Ys leo ingia mwenyewe jikoni ukapike mimi leo sijisikii kuingia jikoni.....shabashiiiii......h apo nani ajiingize kichwa kichwa halafu nije kujutia baadae.......Mr Yes nasema akuuu nimeghairi sitaki tena kukuoa.
HUWAPENDI NDUGU ZANGU,khaaaa hapa ndio kabisa umenivuruga,eti Mr Yes ukinioa mimi sipendi ndugu zako wawe wanakuja kwetu,hasa yule dada yako yule wa Makondeko yuleee.......yani hapo ndio umegusa sehemu nyeti kabisaaa..unajua ni kwa kiasi gani ndugu zangu wamenisaidia mpaka mimi nimefika hapa halafu leo hii unaleta habari za kusaidikika hapa,nasema hapo ndio umegonga ikulu tena sitaki kabisa kusikia neno ndoa kabisaa toka kwako,ndio umenisikia Mr Yes nasema sitaki kabisaaaa,bora uende na mimi nibaki na ndugu zangu maana wao ndio nguzo kwangu.
Mwanamke gani kila siku tu unataka muwe kenye raha na siku shida zinitembelea tu basi ishakuwa dhahama.Eti my baby Mr Yes naomba unitumie shilingi elfu hamsini niende kwa masai nikasuke....sasa hata kama mimi ndio Mr Yes jamani hapo nikihoji tu nywele gani hizo za elfu 50 kosa...."yani we mwanaume kila siku huna hela,un adhani nisingekuwa nahudumiwa ungenikuta hivi?shauri yako usipotunza wenzako watakutunzia",damn,jamani ndio maneno ya kumwambia mwenzi wako hayo?halafu kesho unaomba atimize ile ahadi yake ya ndoa....mhh nimeshtuka mtego huo haunikamati ng'ooo.
Hayo ni baadhi tu yapo mengi tu ambayo mimi Mr Yes yananifanya nisitimize ahadi yangu ya ndoa kwako.Ndoa si mchezo mchezo,ndoa zetu zenyewe za kikristu hizi mpaka kifo kitutenganishe,kwa tabia hizi si ina maana ntavumilia mateso mpaka kifo...aka mimi Mr Yes siajzoea kuishi kwa stress.
Hata kama mzuri zaidi ya Cleopatra lakini kwa tabia hizi nasema kwaheri na mipango ya ndoa ndio imekufa na ninakushukuru ndugu yangu uliyenipa hints zilizonisaidia kumsoma mtu huyu.
Kwa tabia hizi nani akuoe?
Reviewed by CapchaMuzic
on
05:24:00
Rating: