DIAMOND AKAMILISHA ‘TAKEU’ KWA MADEMU
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amekamilisha ‘TAKEU’ kwa mademu baada ya kufanikiwa kutembea na mademu wanaosifika kwa uzuri kutoka Tanzania, Kenya na Uganda.
Historia inaonesha dogo huyo kutoka Tandale aliwahi kufanya kazi na
msanii mrembo kutoka nchini Kenya, Avril na ikadaiwa licha ya kukutana
kikazi jamaa alimsaliti mpenzi wake wa enzi hizo, Penniel Mwingilwa.
Aidha, Diamond amekuwa mpenzi wa Beautiful Onyinye, Wema Sepetu kwa
muda mrefu kabla ya hivi karibuni wawili hao kuamua kupeana likizo.
Katika kukamilisha TAKEU ambayo ni staili ya muziki ya Msanii Nice
Lucas ‘Mr Nice’ inayogusa nchi hizo za Afrika Mashariki, Diamond
juzikati alimnasa mdada anayetisha kwa uzuri na mkwanja nchini Uganda,
Zarinah Hassan ‘Zari’ na kufanya naye project ambapo inadaiwa wawili hao
walivuka mipaka na kupeana penzi.
DIAMOND AKAMILISHA ‘TAKEU’ KWA MADEMU
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:47:00
Rating: