Baba Diamond Amsaka Wema Sepetu, Ataka Kujua Kisa cha Kuachana
Baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ kummwaga mwanaye, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baba mzazi wa jamaa huyo, Abdul Jumaa ‘Baba Diamond’, amenaswa akimsaka mrembo huyo ili kujua mbichi na mbivu.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, baada ya kusikia habari za mwanaye kumwagwa na
Wema aliumia roho kwani anamkubali Wema kuliko warembo wengine wote
ambao walishatembea na mwanaye huyo.
“Hakuna habari mbaya kwa baba Diamond katika kipindi hiki kama ishu ya Wema kumwaga.
MAUMIVU
“Unaambiwa ‘mdingi’ aliumia sana kwani huwa anampenda mkwe wake Wema.
“Baba
Diamond anaamini kabisa kwamba Wema ana nyota ndiyo maana Diamond akiwa
naye huwa anang’ara sana,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
TATIZO NI NINI?
“Amekuwa akimsaka Wema ili ajue tatizo ni nini na kama kuna uwezekano wakae wayamalize.”
Habari
zilieleza kwamba, kwa wiki nzima, baba Diamond amekuwa akimfuata Wema
nyumbani kwake, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar lakini amekuwa
akimkosa.
RISASI JUMAMOSI MZIGONI
Baada
ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili (Risasi Jumamosi) lilipiga kambi
kwa siku kadhaa getini kwa Wema huku likiweka mtego ambao juzikati
ulimnasa mzee huyo.Baba Diamond alishuhudiwa akigonga geti kwenye nyumba
hiyo anayoishi mkwe wake na kuzungumza na mlinzi ambaye alimwambia kuwa
mwanadada huyo hayupo.
Kwa mujibu wa mlinzi wa getini hapo mzee huyo alikuwa akiomba kumuona Wema ili amuulize sababu ya kumwacha Diamond ambaye walikuwa na mapenzi kama ya njiwa.Baada ya kumkosa mzee huyo alisema anaendelea kumsaka hadi atakapompata ili wazungumzie ishu hiyo kiundani.
WAZO LA KWENDA KWA DIAMOND
Baada
ya kuondoka nyumbani hapo kwa Wema, mzee huyo alisema huenda yupo kwa
Diamond na hata kama hatakuwepo itabidi azungumze naye juu ya ishu hiyo
ya kuachwa na Wema.
Ilisemekana kwamba mzee huyo anafanya jitihada zote hizo kwani kwa upande wake Wema ndiye mwanamke pekee anayemkubali.
Ilielezwa kwamba baba Diamond anataka kuwasikiliza kila mmoja na kuhakikisha anawaunganisha upya ili waendelee na safari yao ya kimapenzi hadi watakapooana.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA DIAMOND
Huku
wanahabari wetu wakipeana ishara kuwa wawahi getini kwa Diamond au
Dangote, walipofika mahali hapo, dakika chache baadaye mzee huyo
alinaswa getini kwa mwanaye maeneo ya Sinza-Mori, Dar akigonga mlango.
GETI LAFUNGULIWA
Baada ya
kugonga kwa muda mrefu huku akiwa amefura, alitokea msichana ambaye
alimfungulia mlango mdogo wa getini ambapo alikuwa akizungumza naye
akiomba kuonana na Diamond bila mafanikio.
MAMA DIAMOND KWA MBALI
Wakati
mzee huyo akiomba kuingia ndani, kwa mbali alionekana mama Diamond,
Sanura Kassim ‘Sandra’ kwa mbali akiwa amekaa barazani bila kutambua
sauti ya baba Diamond aliyekuwa akizungumza nje ya geti.
MADANSA WA DIAMOND
Hata
hivyo, baadhi ya madansa wa Diamond walikuwa wakiingia na kutoka bila
kumjali mzee huyo huku mmojawao akimfananisha bila kuwa na uhakika.Baba
Diamond alipoona imeshindikana kumuona mwanaye huku mlango ukifungwa,
aliondoka kwa huzuni akiamini ipo siku atawakutanisha Wema na Diamond
ili kumaliza tofauti zao.
Gazeti hili liliwatafuta zilipendwa hao kwa nyakati tofauti lakini hawakupatikana hivyo jitihada za kuwafikia zinaendelea au hata wao wenyewe wakisoma habari hii watatupigia simu zetu kwani wanazo namba.
TULIKOTOKA
Huko nyuma,
Diamond aliwahi kudai kwamba baba yake alimtelekeza yeye na mama yake
ambapo waliishi maisha ya tabu na kushindwa kusoma kwa kukosa ada lakini
hivi karibuni alitangaza kumsamehe.
Wakati Diamond akifanya kufuru kila kukicha na kugawa magari, baba yake anaishi peke yake, maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar.
Credits:Global Publishers
Baba Diamond Amsaka Wema Sepetu, Ataka Kujua Kisa cha Kuachana
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:45:00
Rating: