Mwalimu wa Makomando wa Jeshi la Tanzania Afanya Mauaji Baada ya Mkewe Kushikwa Kiuno
MWALIMU
wa makomandoo katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha
94 KJ kilichopo Ngerengere mkoani Morogoro, Luteni Octavian Mgowele
(33), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke, Dar es Salaam kwa
tuhuma za kumuua mkazi wa Buza jijini humo aliyetambulika kwa jina moja
la Alkado maarufu kwa jina la Mbavu za Mbwa.
hayo usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, wiki iliyopita wakati akiwa Baa ya Mbondela iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
tukio hilo jana, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, ambaye jina lake
limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake alisema Luteni Mgowele
anayedaiwa kuwa ni komandoo wa JWTZ alikuwa katika baa hiyo na mkewe
ambaye jina lake halijafahamika pamoja na Alkado.
Shuhuda
huyo alisema Mgowele ameoa hivi karibuni walikuwa wamekaa meza moja
pamoja na Alkado wakiendelea kupata vinywaji. Alisema wakati wakiendelea
kupata vinywaji ndipo Mgowele aliponyanyuka na kwenda chooni.
Ilielezwa
kuwa baada ya kurejea alikuta mkewe amehama meza na baada ya kuhoji kwa
nini amehama, ndipo mkewe akajibu kuwa Alkado alikuwa anamshika kiuoni
ndiyo maana amehama eneo alilokuwa wamekaa mwanzoni.
Kwa
mujibu wa shuhuda huyo ni kwamba majibu hayo hayakumfurahisha Mgowele
na akaamua kumvuta Alkado na kisha kuanza kumshambulia kwa kipigo ambapo
alimtoa eneo alilokuwa amekaa na kumsogeza kwenye giza katika eneo hilo
la baa.
Kutokana na kipigo anachodaiwa kupata Alkado
kilisababisha baadhi ya watu waliokuwa kwenye baa hiyo kuingiwa wasiwasi
kuwa huenda akamsababishia kifo. Hata hivyo, hakuna aliyeweza kwenda
kusuluhisha maana mwanajeshi huyo alikuwa akiogopwa hasa kwa kuzingatia
watu wengi wanajua ni komandoo na ni mwalimu wa makomandoo wa JWTZ.
Ilielezwa
kuwa mwanamke aliyetambulika kwa jina la mama Rachel aliambulia kipigo
baada ya kutoa taarifa kuwa kuna mtu anapigwa eneo hilo ambapo mbali ya
kupigwa makofi inadaiwa alimwagiwa mchanga mdomoni kwa sababu ya kusema
kuna mtu anapigwa na mwanajeshi huyo.
Taarifa zaidi zilidai baada ya kipigo hicho, Luteni Mgowele aliamua kuondoka na kuelekea
nyumbani
kwake ndipo wananchi wa eneo hilo walipoamua kutoa taarifa polisi
ambapo walifika na kumchukua Alkado ambaye wakati huo hakuwa na uwezo wa
kuhema kutokana na kipigo alichokipata.
Ilielezwa kuwa
Alkado alifariki dunia eneo hilo la baa baada ya kipigo ambapo kwa
mujibu wa wananchi ni kwamba huenda alichanwa mbavu.
Hata
hivyo, baada ya tukio hilo baadhi ya walinzi katika baa hiyo walisema
Luteni Mgowele alirudi usiku ili kufahamu kinachoendelea lakini mwili wa
Alkado ulikuwa umeondolewa katika baa hiyo ya Mbondele.
Mwili
wa Alkado umehifadhiwa Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam na jana
madaktari wa hospitali hiyo na madaktari wa Jeshi la Polisi walikuwa
wakiufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo.
Akithibitisha
kukamatwa kwa Luteni Mgowele, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Nyigiza
Wankyoo alisema wanamshikilia Mgowele kwa tuhuma za mauaji na kwamba
kesho (leo), hatua zaidi za kisheria zitachukua mkondo wake ikiwa pamoja
na kufikishwa mahakamani.
Alipoulizwa kwa nini asichukuliwe hatua za kijeshi, Kamanda Wankyoo alisema kutokana na
tuhuma ambazo zinatolewa dhidi ya Luteni Mgowele, tuhuma zake zitasikilizwa mahakamani
huku akifafanua jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa wakili wa Serikali.
Kuhusu madai kuwa baadhi ya wanajeshi wamemtorosha mwanajeshi huyo kituo cha polisi,
alisema hazina ukweli wowote na kwamba mwanajeshi huyo anashikiliwa na sheria itachukua mkondo wake.
Kwa
upande wake, Msemaji wa JWTZ , Joseph Masanja alipoulizwa iwapo ana
taarifa za kukamatwa kwa mwalimu huyo wa makomandoo wa jeshi hilo,
alisema hawana taarifa hizo lakini aliahidi kufuatilia ili kubaini kama
zina ukweli au la.
"Hatuna taarifa za tukio hilo,
tutafuatilia na kisha tutatoa taarifa rasmi," alisisitiza wakati
akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu.
Taarifa
zaidi kuhusu tukio hilo, ni kwamba mwili wa marehemu Alkado unatarajiwa
kusafirisha kesho kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.
Kwa sasa msiba upo eneo la Mwembe Yanga, Dar.
Mwalimu wa Makomando wa Jeshi la Tanzania Afanya Mauaji Baada ya Mkewe Kushikwa Kiuno
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:04:00
Rating: