Mama Kanumba afunguka kuhusu skendo yake ya kutembea na Serengeti Boy, hiki ndo alichokisema.
Mayasa Mariwata wa GLobal Publishers
MAMA wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amekanusha vilivyo taarifa zilizozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo ambaye amemzidi umri (serengeti boy).
MAMA wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amekanusha vilivyo taarifa zilizozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo ambaye amemzidi umri (serengeti boy).
Mama Kanumba ambaye pia amefuata nyayo za mwanaye kwa kujiingiza
katika uigizaji, alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na mwanahabari
wetu mambo mbalimbali yahusuyo maisha yake binafsi na sanaa kwa jumla.
Lilipofika suala la tuhuma hizo ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi
ya magazeti (si ya Globa Publishers Ltd) kwamba anatembea na dogodogo,
mzazi huyo alisema taarifa hizo ni za kipuuzi na hazina ukweli wowote.
“Huo ni uongo tu kwa kweli, hakuna kitu kama hicho, mtu mzima kama
mimi naanzaje kufanya vitendo kama hivyo? Heshima yangu itakuwa wapi?”
alihoji mama Kanumba.
Mama hakusita kutoa ufafanuzi zaidi juu ya madai hayo kwenda mbele
hadi kufikia hatua ya kudai kuwa anaonekana na dogodogo huyo katika
maeneo tofauti.
“Wanasema nimekuwa nikionekana naye sehemu tofauti? Inawezekana akawa
ni huyu mwanangu Hotma Peter ambaye nimekuwa nikishirikiana naye kwenye
kazi mbalimbali kwa kuwa watu hawamjui na walizoea kuniona nikiwa na
Seth Bosco (mdogo wa marehemu), ukweli sina bwana na wala sihitaji hata
awe pedeshee wa aina gani,” alisema mama Kanumba.
Akizungumzia kuhusu kampuni ya Kanumba The Great Film aliyoiacha
marehemu mwanaye, mzazi huyo alisema kampuni hiyo kwa sasa bado
inaendeleza shughuli za filamu japo kipindi cha nyuma ilikuwa haipo bize
sana kwa kuwa akili yake haikuwa sawa.
“Kampuni bado inafanya kazi, japo kwa sasa msemaji wa kampuni hiyo ni
Hotma ambaye ni mtoto wa marehemu mdogo wangu, Seth kwa sasa yupo bize
na mambo yake mengine japo tunashirikiana naye katika kuandaa kazi
mbalimbali na tumefanikiwa kutoa filamu moja mpaka sasa.
“Ukweli ni kwamba Kanumba hakuacha kazi yoyote, kwa kuwa kazi zake
zote hatimiliki walikuwa nazo Kampuni ya Steps Entertainment na ya
Mtitu, ni vizuri wasanii wawe makini na hili angalau ziwepo na kampuni
ambazo hazina utaratibu wa aina hiyo wa kumiliki haki zote za kazi ya
msanii,” alifunguka bi mkubwa huyo.
Mama Kanumba afunguka kuhusu skendo yake ya kutembea na Serengeti Boy, hiki ndo alichokisema.
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:27:00
Rating: