Kilichoamuliwa na Mahakama kuhusu kesi ya Chid Benz ni hiki.Picha zaidi ya 10 Zipo hapa

Rapa kutoka La familia Ilala Chid Benz mchana wa October 28 amesimamishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Mashtaka matatu yanayomkabili Chid Benz ni;-
  1. Kukutwa na madawa na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa madawa
  2.  Kusafirisha madawa ya kulevya
  3.  Utumiaji wa madawa ya kulevya
Kwa sasa Chidi Benz amerudishwa rumande hadi Novemba11 ambapo kesi yake itatajwa tena, kuhusu dhamana ya mshtakiwa mahakama imesema itakuwa wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na jumla ya pesa taslim million 1.
chid 4 
Rapper Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam juzi ambapo Mkuu wa Polisi kwenye viwanja vya ndege Tanzania alithibitisha kwamba staa huyu wa hiphop alikutwa na kete 14 alizokiri ni zake za kutumia.
Alikua kwenye safari ya kwenda Mbeya kufanya show lakini ikashindikana manake alibaki mikononi mwa polisi mpaka leo October 28 2014 alipopandishwa Mahakamani Kisutu Dar es salaam kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka matatu ambayo ni kukutwa na dawa na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa dawa, kusafirisha dawa ya kulevya na utumiaji wa dawa za kulevya.
chid 3
Chid 1
chid 2
chid 5
chid 6
chid 7
chid 8
Chid 9
chid 10
chid 11
chid 12
Kilichoamuliwa na Mahakama kuhusu kesi ya Chid Benz ni hiki.Picha zaidi ya 10 Zipo hapa Kilichoamuliwa na Mahakama kuhusu kesi ya Chid Benz ni hiki.Picha zaidi ya 10 Zipo hapa Reviewed by CapchaMuzic on 10:16:00 Rating: 5
Powered by Blogger.