Kabla ya Ommy Dimpoz kua maarufu alikua hiviiii, alikua kachoka mbaya. Cheki picha hapa
Tumetoka mbali! Picha ya staa wa Pozi kwa Pozi ‘PKP’, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, aliyofotolewa enzi anaingia jijini Dar kwa treni imekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wake na sasa inaelekea kutapakaa kila kona ya nchi na wengi wakibishana namna alivyokuwa awali na muonekano wake wa sasa.
Huu ni muonekano wa Staa wa Pozi kwa Pozi, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kwa sasa.
Picha hiyo ambayo ameipiga kitambo juzikati ilisambaa kwa kasi kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii na kuwafanya watu waanze kubishana kama
ni yeye au ni mtu anayefanana naye na wengine kukerwa na picha hiyo
wakisema itolewe kwa kuwa inamdhalilisha staa wao.
Baada ya kuona mzozo huo unakuwa mkubwa, gazeti hili lilimtafuta Ommy
Dimpoz ili aeleze kama ni yeye ambapo alikiri kwamba ni yeye na kudai
aliyekuwa na picha hiyo ni mjomba’ake tu anashangaa ilivyovuja
mitandaoni.
Stori: Musa Mateja wa Global Publisher
Kabla ya Ommy Dimpoz kua maarufu alikua hiviiii, alikua kachoka mbaya. Cheki picha hapa
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:51:00
Rating: