Chupuchupu Kubakwa, Kusingizia Nina Ukimwi ilinisaidia
Habar ya humu wadada na wakaka... Wakubwa na wadogo kwa ujumla..
Nimekumbuka
hili tukio lililonitokea kitambo kidogo japo si sana lakini bado
nakumbuka na ningependa kushare na ninyi hapa..najua jf ina watu wengi
na wa umri mbalimbali tunaweza kusaidiana kinamna moja ama nyingine"..
Nakumbuka
siku ya tukio nilipokea simu namba mpya na jamaa alijitambulisha kama
"Michael", sikumfahamu awali ila aliniomba niwe mpole nitamfahamu
polepole na jioni yake aliniomba tule dinner wote sikubisha!".. Jioni ya
saa moja niliweka mambo yangu vizur na kujiandaa mpaka saa mbili Tayar
kulikuwa Giza,nikajivalia kigauni cha usiku kilichoacha sehemu kubwa ya
mapaja yangu wazi!.nilichukua pikipiki mpaka sehemu husika (jina
sipakumbuki vizuri), baada ya kushuka kwel nilimuona lkn bado
sikumfahamu..tulikaa sehemu kuna kagiza taa kwa mbali hatukuongea sana
akaniuliza ntakula nn nikamwambia..chakula kikaletwa tukala tukashiba
akaniambia hakai mbali na pale tulipo ivo twende kwake aliniandalia
kinywaji..nikakubali tukaenda. Kiukwel hapakuwa mbali kama kupanga basi
alijipanga vyema...
Tulipofika
aliniwekea Bia mbili za Safari baridi..sikuwa na mzuka sana siku hiyo
na ivo alitegemea ningelewa mpaka nisijiweze lkn haikuwa ivo kwan zile
bia zilinifanya niwe na nguvu zaid..baada ya mda kwenda ilitimu saa nne
nikamuomba kuondoka ndo tatizo lilipoanzia hapo...akataka tufanye
mapenzi tena kwa lazima nikagoma...tulibishana na kuvutana akaona namzid
nguvu huku mda unazid kwenda...mungu anisamehe maana nilipata wazo la
kumcoma kisu nikimbie lkn alilock mlango na ufunguo akautupa chini ya
uvungu..baada ya mda nilisikia anaongea na simu aliporud akaniambia si
najifanya mjanja sitaki kumpa papuchi basi nitaitoa kwa lazima..mara
nilisikia group la wanaume weng kwa nnje wakigonga wafunguliwe hapo
pombe yote ilipotea kichwan nikajikuta nasmile huku nawaza cha
kufanya..nilimvuta taratibu nikamuigizia uwoya haoni
ndani...nilimbembeleza kama motto kwa sauti ya kimahaba sana huku
machozi yakinitoka..nilisingizia ukimwi huku namuangalia usoni kama kwel
vile..alinyong'on yea akaniamni.aliwatoa wale wanaume akanirudisha
nilipokuwa nakaa saa tano akinishukuru njia nzima.nilifika na kulala
tu...
Wanaume
nawaheshimu lkn sijui nawaonaje..bado weng wenu mnatakiwa kujifunza
mengi juu ya mwanamke...ni kiumbe adimu hlf mapenzi sio amri ni hisia
.kwa wale wapenda ofa na kukutana na mastrangers angalieni sana
yasijetokea puani.
Usikuni mwema.
Chupuchupu Kubakwa, Kusingizia Nina Ukimwi ilinisaidia
Reviewed by Unknown
on
02:48:00
Rating: