Chuchu Hans afungukia juu ya ndoa yake na Ray
BAADA ya minong’ono ya muda mrefu katika vyombo vya habari
kuhusu uhusiano wa kimapenzi baina ya wasanii nyota wa filamu za Bongo;
Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’, hatimaye Chuchu ameweka wazi suala
la ndoa yao.
Chuchu amekiri kwamba wao ni wachumba na wakati
wowote Mungu akiwajalia wanaweza kufunga ndoa na wameamua suala la
tofauti za dini baina yao wameliacha kwa wazazi wao.
“Sisi ni watu wazima, tunajua tunachokifanya. Ni
kweli mimi na Ray ni wachumba na ninampenda ‘baby’ wangu. Ukifika wakati
tutafunga ndoa rasmi, suala la dini ni la kukaa familia na kupanga
tufunge kwa dini gani,” alisema Chuchu.
“Hata hivyo, hilo ni suala langu binafsi kuamua
kufunga ndoa kwa dini gani lakini tunawaachia wanafamilia wachague na
kupanga, kwa sasa ni mapema mno kusema tutafunga ndoa ya Kiislamu au
Kikristo.”
Uhusiano wa wasanii hao umekuwa gumzo katika
tasnia ya filamu na ilifika wakati uvumi ulidai kwamba Ray alishabadili
dini na kuchagua jina la Aboubakary ili aweze kufunga ndoa ya Kiislamu
na Chuchu.
Chuchu hakutaka kuingia ndani kuhusu hilo na kusisitiza kwamba wazazi wao ndio watakaoamua wafunge ndoa kwa dini gani.
Ray ni Mkristo na Chuchu ni binti wa Kiislamu na
wazazi wao wameshiba dini hali inayofanya wengi kutaka kujua ni nani
atabadili dini au kama watafunga ndoa ya kiserikali.
Chuchu Hans afungukia juu ya ndoa yake na Ray
Reviewed by CapchaMuzic
on
05:50:00
Rating: