BAADA YA KHARIBU UJERUMANI DIAMOND ATIA AIBU NYINGINE DODOMA!
KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.
Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.
AIBU YENYEWE
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.

MAFUNDI MITAMBO WAHAHA
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.

Muda
mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka
tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha
mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.
WEMA ATAKIWA
Katika zomeazomea ya safari hii, mashabiki walikwenda mbele zaidi wakimtaka Wema apande jukwaani kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.

Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.
MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.

Kitendo
hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama
muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye
maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha
shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.
“Haiwezekani
bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo,
unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka
betri mpya kwenye maiki?
DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila mara huku maiki nazo zikikoroma.

“Braza
huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye vigodoro lakini
siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu wameingia kwa bei
mbaya, ni kuwaibia watu.
“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond.

INTAVYUU FUPI
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo. alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana ni Diamond.

UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31, mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart.

Nchini
Uingereza nako, Septemba 20, mwaka huu, Diamond alijikuta ndani ya aibu
kubwa kwa mashabiki wake kufuatia mwandaaji kuingia mitini katika
ukumbi wa LafACE club jijini Londan licha ya mashabiki kujaa.
KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana.

Kwa
kawaida, msanii anapokwenda kupiga shoo mahali, kuna utaratibu unaoitwa
kwa Kiingereza kama Technical Rider ambapo wasimamizi wake, akiwemo
meneja huenda kuukagua ukumbi, usalama, muziki wenye viwango na hata
steji shoo ilivyo.
Kama
mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo. Lakini
mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa makubaliano.Meneja wa
Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili kuulizwa kwa nini hakuwepo
Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki na maandalizi mengine,
hakupatikana hewani!
BAADA YA KHARIBU UJERUMANI DIAMOND ATIA AIBU NYINGINE DODOMA!
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:41:00
Rating: 5