VILIO NA MACHOZI VYATAWALA UPYA KWENYE KABURI LA RECHO
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Roho inauma! Kwa mara
nyingine, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel Leo
Haule ‘Recho’ (pichani) limeloa machozi ya mastaa wakati wa kusimikwa
msalaba baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa, Ijumaa Wikienda
lilikuwepo.
Katika tukio hilo lililojiri wikiendi iliyopita, vilio vya mastaa
vilianzia Kanisa la Anglikana lililopo Magomeni-Mwembe Chai, Dar ambapo
ilifanyika ibada maalum kwa ajili ya kumuombea marehemu huyo na wengine
waliotangulia mbele ya haki.
Ibada hiyo iliyoambatana na kuombewa na kutakaswa kwa msalaba huo,
iliongozwa na Mchungaji Mtweve na baadaye walielekea Makaburi ya
Kinondoni, Dar lilipo kaburi alilopumzishwa Recho.
Walipofika makaburini, mastaa hao walijikuta wakiangua vilio huku baadhi yao wakizimia kwa kumkumbuka mpendwa wao.
Walipofika makaburini, mastaa hao walijikuta wakiangua vilio huku baadhi yao wakizimia kwa kumkumbuka mpendwa wao.
Tofauti na mastaa wengine, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Blandina Chagula ‘Johari’ walipitiliza kwa kulia kwa sauti kubwa.
Kuna wakati Odama alishindwa kuvumilia kulisogelea kaburi kwani
aliangua kilio kilichosababisha mama wa Bongo Muvi, Herieth Chumila
kumzuia kwa kuhofia kuishiwa nguvu.Mwisho, Odama na aliyekuwa mchumba wa
Recho, Saguda George walitoa neno la shukrani kwa watu wote waliofika
eneo hilo na kuomba ushirikiano kwa lolote litakalotokea.
Nayo familia ya Recho, iliwapongeza Odama na Saguda kwa kuwa na moyo
wa upendo kwa marehemu tangu alipoumwa mpaka alipoaga dunia hadi
kumjengea kaburi na kuwaomba waendelee kushirikiana kwa ajili ya umoja
waliounganishwa na Recho.
Mbali na Odama, Johari, Herieth na Saguda, baadhi ya mastaa wengine
ni pamoja na Steve Nyerere, Mike Sangu, Najma, Lamata, Kupa na wengine
kibao.Recho (26) alifariki dunia Mei 25, mwaka huu wakati ajikifungua
ambapo kichanga chake nacho kiliaga dunia
VILIO NA MACHOZI VYATAWALA UPYA KWENYE KABURI LA RECHO
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:25:00
Rating: