Unaweza kumuelezea Diamond Platnumz hivi….
HeartBreaker
Kwanza tunaanza na nyimbo zake yeye mwenyewe. Nyimbo zake nyingi
ameandika kutokana na historia ya kweli iliyowahi kumtokea na ikiwa ni
kuumizwa na wapenzi wake wa zamani au yeye kuwapiga vibuti. Nyimbo ya
mawazo na kamwambie ni nyimbo yenye hisia kali aliyomwandikia demu mmoja
anayeitwa sara aliyempiga kibuti na kuolewa na mtu mwenye pesa. Nyimbo
ya mawazo alimuimbia jackline wolper , huku nyimbo ya ukimwona akiimba
kupeleka ujumbe kwa demu wake wa sasa wema sepetu ambapo kipindi hicho
ndio alikua amepigwa kibuti. Ukiachana na hao diamond ashawahi kua na
mahusiano na demu penny na jokate mwengelo.
Hit Maker
Diamond ameshaandika nyimbo zaidi ya 133 . Diamond anacharge zaidi ya
milioni 6 kwa show za ndani na dollar 25,000 kwa show za nje.Miaka
miwili iliyopita alifanya show kigali , Rwanda na kupata 100,000 US
dollars.
Money Maker
Utajiri wa diamond unakadiriwa shillingi billioni 1.2 . Diamond
Platnumz amewekeza kwenye Real Estate na anapangisha nyumba kadhaa hapa
mjini. Ana Clothing line yake, ana miliki fashion boutiques , viwanja
vya kutosha na magari ambayo ukijumlisha gharama yake unajena hoteli ya
nyota 4. Pia Ana mikataba mikubwa yakibiashara na Vodacom na Coca-cola.
Unaweza kumuelezea Diamond Platnumz hivi….
Reviewed by CapchaMuzic
on
11:16:00
Rating: