Ukiona haya , jua ushazama kimapenzi….
Hauwezi kuacha kufikiria kuhusu yeye
Muda wote utakua unafikiria kuhusu yeye, kuhusu mipango uliyopanga naye,maisha ya baadae na mengineyo.
Unamjali
Kuna sababu ambazo watu hua hawawaulizi au kuwatafuta wenzao ambao
walikutana usiku mmoja na ku-have good time,ni sababu
hawajawapenda.Ukiwa in love utataka kujua kila kitu kuhusu mwezako,yeye
ni nani,anafikiria nini, kitu gani kitamfanya afurahi .Unajali kwa
ukweli hisia zake.Kama unampenda mtu kweli hautajisikia vizuri anapokua
na siku mbaya au tu amekasirika kutokana na jambo fulani.
Ni Mkamilifu
watu wanaopendana huwa wanaangalia mambo mazuri kuhusu wenzao huku wakiyapotezea mapungufu mtu aliyonayo.
unataka akue
Unapotaka mwenzi wako apambane na changamoto mbalimbali ili aweze
kukua as a person. Kama unataka mwenzako abaki hivyohivyo na asijaribu
vitu vipya basi hapo hamna upendo.
Mna Chemistry nzuri
Hii ni hali ya kufikiria na kutenda kwa upeo mmoja, na kufikiria
mawazo yanayofanana au wote kupenda vitu vinavyofanana kama wote kupenda
kuogelea,muziki au kusafiri.
Unapenda kutumia muda wako nae
Hii ni jambo lililo wazi lakini ni la muhimu sana.Unasubiri kwa hamu
kumuona na kukutana nae huku kutojali kihivyo mtautumiaje muda
huo,unachojali ni kuonana nae.Usipokua nae pamoja unam-miss na kutamani
angekua nawe.
Unaweza Kuishi na Mapungufu yake
labda ni jasho lake linavyotema akitoka mazoezini au hasira kali
aliyonayo anapokasirika na bado ukaweza kukubaliana na hali hii ni
ishara tosha ya upendo halisi kwa mwenza wako.
Vipaumbele vingine vinakuja baadae
kawaida unatumia muda fulani kwenda mazoezini lakini anapotaka kwenda
dinner basi haitakua tabu kwako kubadilisha ratiba zako na kutoka naye.
Kufanya chochote kwa ajili yake
watu wanaopendana wapo radhi kufanya jambo lolote kwa ajili ya mwenza wako hata kufa kwa ajili yake.
Unaanza kufikiria maisha yako ya baadae na yeye anakwepo
Unapoweza kumuweka kwenye picha yako ya miaka mitano,kumi au hata
hamsini mwenza wako basi hiyo ni ishara tosha kwamba unampenda.
Ukiona haya , jua ushazama kimapenzi….
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:51:00
Rating: