Siri imefichuka Kuuungua kwa Bigg Brother kumbe ni kutafuta "kiki"...
Ni kweli jumba la Big Brother Africa lililopo jijini Johannesburg,
Afrika Kusini limeungua? Ni kweli msimu wa tisa uitwao Hotshots
hautazinduliwa Jumapili kama ilivyopangwa? Hayo ni maswali mawili
makubwa wapenzi wa shindano hilo maarufu barani Afrika wanaendelea
kujiuliza hadi sasa bila kupata majibu.
Uhalisia ni kwamba wengi wameiamini habari hii hasa kwakuwa imeandikwa na vyombo vya habari wanavyoviamini na pia waandaji, M-Net na Endemol South Africa wao wenyewe wamethibitisha kutokea kwa moto huo na kueleza kuwa uzinduzi wa msimu wa tisa umeahirishwa hadi pale watakapotangaza tena.
Jamaa wanadai kuwa wanatafuta nyumba nyingine itakayofungwa camera zingine na popote ilipo duniani na kama itakuwa na vigezo wataichukua ili msimu uanze. Moto huo unaodaiwa kuwa mkubwa umepelekea kuharibika kwa camera maalum 56 hivyo waandaji wanatafuta nyumba nyingine Big Brother popote duniani ambapo washiriki watasafirishwa.
“M-Net na Endemol SA wana timu nzima inayotafuta mbadala wa nyumba nyingine ya Big Brother Africa,” Caroline Creasy kutoka MultiChoice Africa ameiambia Channel24. “Hii inajumuisha kutafuta nyumba za Big Brother kwingine duniani ambazo zinaweza kuwa wazi kwaajili ya utayarishaji.”. “Katika hatua hii hakuna uamuzi wa mwisho uliochukuliwa kuhusiana na nyumba au muda utakaowahi. Timu inafanya kazi saa 24 kutafuta suluhu ya kuipeleka show hewani,” aliongeza.
Wanasema kuhama nyumba kunamaanisha si tu kusafirisha washiriki bali pia crew nzima ya watayarishaji na awamu nyingine ya kuonba visa na mabadiliko pamoja na kuagiza vifaa vipya.
Kwa maelezo hayo, ni rahisi kuamini habari hii kuwa ni ya kweli na kwa wapenzi wengi wa show hiyo, hii imekuwa habari mbaya wiki hii. Hata hivyo kuna sababu kadhaa ambazo ukizifirikia kwa umakini, ni rahisi kuingiwa mashaka na ukweli wa tukio hilo. Ni kweli ama ni kiki tu?
Big Brother Africa ni mchezo tu, hivyo chochote kinaweza kufanyika na katika masuala ya burudani kutafuta kiki au Publicity Stunt hata kwa mambo ya uongo ni mambo yanayotokea.
Kwa kiasi kikubwa mimi naamini kuwa habari ya moto na kuahirishwa kwa uzinduzi imepikwa na waandaaji kutengeneza hamu, mshtuko na kuhype zaidi uzinduzi wake.
Publicity Stunt ni kitu cha kawaida kwenye tasnia ya burudani duniani. Unakumbuka September 2007, 50 Cent aliwahi kudai kuwa angestaafu muziki kama album yake, Curtis, ingezidiwa mauzo na album ya Kanye West, Graduation! Alitoa kauli hiyo wiki chache kabla ya kufika siku ambayo album hizo zilikuwa zizinduliwe.
Kweli, album ya Kanye iliuza kopi zaidi ya kopi 957,000 kwenye wiki yake ya kwanza na Curtis kuuza kopi, 691,000. Lakini 50 hakustaafu. Baadaye alikuja kukiri kuwa hiyo ilikuwa ni publicity stunt na kweli ilimsaidia.
Kwanini nadhani issue ya BBA ni Publicity Stunt?
Kwanza, suala la moto katika jumba la thamani kama la BBA ambamo kuna samani za thamani, vifaa vya electronics kama camera zilizonunuliwa kwa bei ghali si suala la mzaha. Kama kweli jumba hilo lingekuwa limeungua, tungeoneshwa picha nyingi za namna moto huo ulivyoliteketeza. Picha zinazooneshwa ni chache na ni zilezile.
Tungeoneshwa picha za ndani kuona hasara iliyopatikana na jinsi moto ulivyochoma vifaa hivyo vya thamani. Vituo vikubwa vya runinga vingefunga kambi kwenye jumba hilo kuelezea ukubwa wa moto huo, wangehoji wahusika ambao wangeeleza hali ilivyokuwa na mambo mengine. Hivyo ndivyo kwenye matukio mengine makubwa ya moto hufanyika. Ni wapi umeona video inayoonesha jumba likiwa limeungua? Hakuna waliorekodi?
Hushangai kwanini picha za jumba linalodai kuungua ni zilezile hadi leo, hakuna mpya? Pia zichunguze vizuri picha za nyumba inayoungua na utagundua kuwa hicho ni kiwanda na sio nyumba yenye hadhi ya kuwa Big Brother. Kwa kawaida na kwa ukubwa wa BBA, nyumba wanayowekwa washiriki hao huwa ni nyumba ambazo kama ni Dar es Salaam basi ni zile zinazopatikana kwenye maeneo ya kishua kama Masaki, Oysterbay au Mbezi Beach. Kwa picha hizo zilizosambaa mtandaoni kuwa ni jumba la BBA lililoungua, utagundua kuwa nyumba hiyo ipo eneo wanapoishi watu wa kawaida kabisa nchini Afrika Kusini. Huwezi kufunga vitu vya thamani kwenye godown hilo.
BBA House au kiwanda cha mikate? Moja ya picha inayodaiwa kuwa ni jumba la Big Brother Africa lililoungua
Pili kwa jinsi ambavyo wao wenyewe M-Net waliwahi mno kulitangaza tukio la moto, imeonesha wazi kuwa ni tukio lililopangwa na wao wenyewe. Kwa kawaida, kampuni au taasisi inapopata ajali ya moto kama hiyo, huchukua muda kutafakari na kubaini hasara iliyotokea kabla ya kuamua kuongea na waandishi wa habari. Kamwe, huwezi kuwahi kuongea baada ya kupata hasara kubwa kama hiyo.
Tukio la moto lingekuwa la kweli, ingekuwachukua siku mbili hadi tatu kuongea na tena wangeita waandishi wa habari kuzungumzia. Kinaonekana kimefanyika ni kuwa M-Net wamezungumza na blogs/magazeti machache yenye nguvu Afrika Kusini kusaidia kueneza ‘kiki’ hii kwa makubaliano maalum yakiwemo malipo na vyombo vingine vya habari duniani vingekopi tu kutoka kwao, na ndio hicho kilichofanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kiki imekiki.
Tatu, ni picha za mameneja wa Diamond Platnumz ambao huenda wakawa wamechangia kuharibu stunt hii ya BBA. Kama uzinduzi huo umeahirishwa kufanyika Jumapili hii kama ilivyokuwa imepangwa, Diamond na timu yake waliopangwa kutumbuiza wanaenda kufanya nini Afrika Kusini?
Hawa jamaa wanaenda kufanya nini Afrika Kusini wakati uzinduzi wa Hotshots Jumapili hii ambako Diamond atatumbuiza umeahirishwa?
Nne, ni kuendelea kuchezwa kwa promo inayoelezea uzinduzi wa show hiyo kwenye vituo vya TV vya Multi Choice. Jana nilikuwa naangalia kituo cha Movie Magic Swahili na mara kadhaa nimeona promo hiyo inayoelezea uzinduzi wa Hotshots wa September 7 ikichezwa kama kawaida.
Hiki ndicho M-Net watafanya:
Kwakuwa stunt hii imetengenezwa kwa umakini mkubwa, waandaji wa show hiyo tayari wametengeneza mazingira ya kuja kutoa tamko kabla ya Jumapili kuwa wamepata mbadala wa nyumba nyingine na uzinduzi huo utaendelea kama kawaida. Na ndio maana wanasisitiza kwa kusema ‘the team is working around the clock to find solutions to get the show on-air’.
Pamoja na kubaini kuwa hii ni publicity stunt, tukumbuke kuwa BBA si kombe la dunia au mashindano ya Olimpiki. BBA ni mchezo wa burudani na kwakuwa burudani na kiki ni kama kaka na dada hili ni jambo la akili M-Net wamelifanya mwaka huu kuhype na kutengeneza hamu zaidi ya shindano hilo. Ama pengine ndio maana linaitwa ‘Hotshots’ yaani ni shot za moto kwa kwenda mbele… Acha tusubiri tuone na ntakuwa tayari kuwa proved wrong..
Adios!!

Reviewed by CapchaMuzic
on
02:05:00
Rating: