PICHA;YALIYOJIRI KWENYE KICHENI PATI YA LUCY KOMBA....NI SHEEDA
Stori: Imelda Mtema
NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida,
wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo
Movies walihudhuria.
Miongoni
mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi
mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye
magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku
miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa
nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika
nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.
Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake
ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani
alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania
huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake
alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika
mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake.
Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara
ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni
waalikwa.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji
kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha
alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na
wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake
aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na
baadaye kuangusha nyingine Denmark.
PICHA;YALIYOJIRI KWENYE KICHENI PATI YA LUCY KOMBA....NI SHEEDA
Reviewed by CapchaMuzic
on
01:15:00
Rating: