PENZI LA MSANII KUTOKA NIGERIA LAMLEVYA JOKATE!
Ikiwa imepita wiki kadhaa tangu mrenbo Jokate Mwegelo 'Kidoti' akutanishwe na Mwanamuziki wa Nigeria Ice Prince kwa aajili ya kurekodi kipindi cha luninga cha Channel O nhini Afrika kusini,kwa sasa wawili hao wameanza kuhisiwa kuingia mapenzini.
Jokate ambaye kwa sasa yuko Afrika kusini,kwa siku za karibuni ameonekana akipachika kwenye tovuti ya Instagram,Picha na Video kadhaa zinazomwonyesha mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo wa Iswear.
katika moja ya Video inamwonyesha akizungumza na mwanamuziki huyo tovuti ya Skype,huku baadhi ya maneno ya maneno ya maongezi yao kuonekana kufutwa na zaidi mwanamuziki huyo akisikika akilitaja kwa usahihi jina la kidoti.
kwa kiasi kikubwa Jokate alifurahishwa mno na utamkwaji wa usahihi wa jina lake na mwanamuziki huyo wa Rap,na kufurahia zaidi alipoelezwa kuwa'amemmisi' sana.
kwa kile kilichoonekana kuwa ni Jokate'kudata'kwa Ice Prince,ni jinsi alivyo na kasi kubwa ya kupachika mtandaoni picha wakiwa pamoja lakini kwa mwanamziki huyo imekuwa tofauti.
Aidha,wiki chache zilizopita Jokate aliwaikuweka wazi juu ya kuchoshwa kwake na maisha ya kutokuwa na mpenzi na badala yake kuhitaji kupata mpenzi atakaye kuwa mumewe hapo aadae
-->
PENZI LA MSANII KUTOKA NIGERIA LAMLEVYA JOKATE!
Reviewed by CapchaMuzic
on
05:37:00
Rating: