Ney wamtego akiri kujiusisha na Freemason asema anachoangalia ni maslahi zaidi
Rapper Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni alizusha maneno mengi
kutokana na video ya wimbo wake ‘Mr Nay’ yenye mambo ya kutisha,
amewajibu mashabiki wake kwamba hajali kuhusishwa na ufreemason ilimradi
anaingiza pesa anayoitaka.
Akizungumza
na kituo cha redio cha Victoria FM kilichopo mjini Musoma, Nay amesema
amekuwa akipokea maswali mengi yakitaka kujua kama anajihusisha na jamii
ya siri ya freemason kutokana na matendo yake.
“Mimi sijali kama
najihusisha na freemason, naangalia jinsi gani naingiza pesa na huu
ndio aina ya muziki wangu na kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. Muziki
wangu na maisha yangu kama yanahusishwa na freemason lakini ninachojali
ni pesa tu,” alisema.
Ney wamtego akiri kujiusisha na Freemason asema anachoangalia ni maslahi zaidi
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:46:00
Rating: