MSIBA WAZIMA MBWEMBWE ZA AUNT MAREKANI
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata
alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake
aliyefariki dunia juzikati.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za mdogo
wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki
dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye
mazishi.
Ijumaa lilipata bahati ya kuwasiliana na Aunt ambaye alisema
ameshitushwa na taarifa hizo na alikuwa njiani kurejea Dar.“Nimeumia
sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu tuliyependana sana lakini Mungu
kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa masikitiko.
MSIBA WAZIMA MBWEMBWE ZA AUNT MAREKANI
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:34:00
Rating: