KIJANA HUYU AUAWA KWA KUCHOMWA VITU KICHWANI NA KIFUANI AKITUHUMIWA KUWAROGA WATOTO NA KUTUMIKISHA WATU KICHAWI

Marehemu
Gabriel Mwandemwa(Mwasyebule) enzi za uhai wake, Marehemu alikuwa
akijishughulisha na biashara mbali mbali ikiwemo uuzaji wa maziwa na
ununuzi wa mahindi.
Matukio
ya wananchi kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi
ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio la jana kijana wa miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo
hicho na kumtaja marehemu kuwa ni Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi
wa kijiji cha Ikamambande Wilaya ya Rungwe.
Alisema kijana huyo aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema
tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tano asubuhi huko katika Kijiji
cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe,
mkoani Mbeya.
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo uliitisha
kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na
ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika
kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema
marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa
anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi kwa kuwatumikisha watu
kishirikina.
KIJANA HUYU AUAWA KWA KUCHOMWA VITU KICHWANI NA KIFUANI AKITUHUMIWA KUWAROGA WATOTO NA KUTUMIKISHA WATU KICHAWI
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:45:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
10:45:00
Rating: