Jack Patrick Atuma Ujumbe Mzito Kwa Watanzania Huku Akiwa Gerezani China
Stori: Imelda Mtema
MWANAMITINDO wa Bongo aliyepo nyuma ya nondo huko Macau, Hong Kong
nchini China akitumikia kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia
ya kubeba madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack
Patrick’ ametuma ujumbe mzito kwa mashabiki wake.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, rafiki wa karibu wa Jack ambaye
hakupenda jina lichorwe gazetini, alisema kwamba mwanamitindo huyo
amekuwa akimuandikia barua mara kwa mara lakini safari hii ametaka
ujumbe wake uwafikie Watanzania.
“Amesema watu wasimhurumie kuhusu kufungwa, amesisitiza sana juu ya
suala mavazi na mitindo. Amesema hapendi kuona Tanzania inayumba katika
masuala ya mitindo ambayo yeye alikuwa akiiamini kwamba ni kazi ambayo
inaweza kuwaingizia kipato watu wengi,” alisema rafiki huyo wa karibu.
Rafiki huyo alizidi kuweka wazi kuwa mara nyingi Jack hapendi kuwaambia
juu ya maisha ya jela kwani hapendi kabisa kuwapa watu simanzi bali
anapenda watu wajue anaishi maisha ya kawaida.
“Mara nyingi Jack hapendi kabisa kueleza maisha ya jela, hapendi
kuwaumiza wat, anachopenda ni kujua nini kinachoendelea katika fasheni,”
alisema rafiki huyo wa Jack.
Rafiki huyo alisema kuwa Jack bado anaagiza nguo ambazo alikuwa akipenda
kuvaa hasa lineni nyeupe na kuwataka watu wahisi kama yupo masomoni na
atarejea tu akiwa salama.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya
aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau
akitokea Bangkok, Thailand kuelekea Guangzhou, China.
GPL
Jack Patrick Atuma Ujumbe Mzito Kwa Watanzania Huku Akiwa Gerezani China
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:25:00
Rating:
Reviewed by CapchaMuzic
on
02:25:00
Rating:
