Breaking Newz; Kifaru cha Pinduka ahsubuhi hii na kuuwa wanajeshi na raia Lindi
Kutoka
Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga kuhusu
ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la Wananchi
Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo na shuhuda wa eneo hilo.
Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara kuelekea Nachingwea
kwenye camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo ya Mnolela
kijijini Lindi,kwa mujibu wa shuhuda ambaye ametoa taarifa hii kupitia
kipindi cha Power Breakfast kutoka Clouds Fm amesema ajali hiyo imeua
wanajeshi 3 na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua kalala
ndani.
Madhara mengine yaliyotokana na ajali hii ni nyumba mbili kuharibika
vibaya,majeruhi wa ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa
Mtwara.
Bonyeza play kumsikiliza shuhuda wa ajali hii.
Breaking Newz; Kifaru cha Pinduka ahsubuhi hii na kuuwa wanajeshi na raia Lindi
Reviewed by CapchaMuzic
on
23:53:00
Rating: