ALIYEZAA NA RIYAMA ANASWA!
Hakuna
siri ya wawili duniani! Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Riyama Ally
kumfichaficha mwanaume aliyezaa naye kwa muda mrefu, hatimaye jamaa
huyo amenaswa.
Tukio hilo lililopigwa chabo na ‘mtu wetu’ lilijiri wikiendi
iliyopita kwenye Ukumbi wa Chabruma uliopo Mabibo, Dar ambako kulikuwa
na bethidei ya mtoto wa Riyama aitwaye Fatuma aliyetimiza miaka miwili
ambapo alifanya sherehe kama harusi huku akiunganisha na bethidei yake
iliyokuwa siku moja kabla ambapo mastaa kadhaa walihudhuria.
Muda mfupi baada ya Riyama na mwanaye kuingia ukumbini, waliofuatia
kuingia huku wakicheza muziki kwa staili ya Kisambaa walikuwa ni wakwe,
yaani baba wa mtoto na mama yake na ndugu wengine waliowasindikiza.
Baada ya kuingia, sherehe ilianza ambapo mshehereshaji ambaye ni
msanii wa filamu, MC Kinyata alimwita mbele baba wa mtoto anayejulikana
kwa jina moja la Haggy na kuungana na mzazi mwenzake na mtoto wao na
hapo zoezi la kukata na kulisha keki likaanza.
Wawili hao walionekana wenye furaha huku wakilishana keki na
kukumbatiana kimalovee hali iliyosababisha ukumbi ulipuke kwa vigelegele
na baada ya hapo walikuwa pamoja hadi mwisho wa sherehe.
ALIYEZAA NA RIYAMA ANASWA!
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:04:00
Rating: