AJALI MUSOMA YADAIWA NI KAFARA!
Stori: Musa Mateja aliyekuwa Mara
Inauma sana!
Ajali mbaya iliyosababisha vifo vya watu 39 iliyohusisha Basi la
Kampuni ya J4 Express lenye nambari za usajili T 677 CYC, lililokuwa
likitoka Musoma kuelekea Sirari mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa
uso na basi lingine la Kampuni ya Mwanza Coach lenye nambari za usajili T
736 AWJ katika eneo la Saba Saba mjini Musoma mkoani Mara, Ijumaa
iliyopita, imedaiwa kuna ushirikina au kafara ndani yake.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo waliliambia Ijumaa Wikienda kwamba
kuna kafara ilitolewa na mmoja wa watu waliohusika katika ajali
hiyo.“Haiwezekani magari yakagongana uso kwa uso sehemu nyeupe kama ile,
hata kama ni uzembe, ajali hii ni zaidi ya uzembe,” alisema kijana
mmoja aliyeshuhudia ajali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa imani
hiyo ya kishirikina.
Aliongeza kwamba kuna wafanyabiashara wengi walikuwa kwenye mabasi hayo na baadhi yao wanapenda mambo ya kishirikina.
Baadhi ya miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo.
Hata hivyo, alipobanwa zaidi, hakuwa tayari kutoa ufafanuzi.
Shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Maduhu alidai kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kulipita
gari dogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK
katika sehemu ambayo mbele kulikuwa na daraja linaloweza kupitisha gari
moja kwa wakati mmoja.
Guldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
namba ya usajili T 332 AKK lililosukumwa na basi kwenye ajali hiyo mpaka
kuingia mtoni. Gari hili ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili
wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
“Ukweli wapo watu wanadai kuwa hii ni kafara ili majini wanywe damu
na mambo yao yaende vizuri lakini ukweli ni kwamba basi hilo lilikuwa
kwenye mwendo kasi, lililisukuma ubavuni gari dogo ambalo halikuweza
kuhimili na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni nalo kugongana na
basi la Mwanza,” alisema Maduhu.
Jumamosi iliyopita, gazeti hili lilipokea ripoti kuwa bado
haijafahamika ndani ya mabasi hayo kulikuwa na abiria wangapi ambapo
ilidaiwa kuwa waliokufa na majeruhi walikuwa wameongezeka.
AJALI MUSOMA YADAIWA NI KAFARA!
Reviewed by CapchaMuzic
on
00:50:00
Rating: